Wednesday, September 25, 2013

Papa Benedict akanusha kutokuwajibika kwa kashfa za Kanisa.

Pope Benedict XVI gives a blessing during the Angelus prayer from the window of his summer residence of Castel Gandolfo August 12, 2012. REUTERS/Giampiero Sposito (ITALY - Tags: RELIGION) - RTR36QX4
                                                                                   Papa Benedicte XVI azuru Benin
Papa wa zamani Benedict ameibuka kutoka kwenye ukimya binafsi   ndani ya Vatican na kukanusha  hadharani kwamba alificha vitendo vya manyanyaso ya kingono kwa watoto na mapadri wa kanisa katoliki.
Katika barua ndefu kwa mtunzi wa vitabu wa Italia asiye na dini na mwanamahesabu (Piergiorgio  Odifredi) na kuchapishwa jana Jumanne na gazeti la La Republica , Benedict alikana kutokuwajibika kwa kashfa ya ngono kwa watoto.Lakini amesema kanisa  lazima lifanye kila iwezalo kuzuia vitendo kama hivyo kutokea tena.

Makundi ya waathirika wamemshutumu Papa huyo kwa kutokufanya vya kutosha kuzuia manyanyaso hayo, kabla ya kuwa Papa na baada , wakati alipoongoza ofisi ya kanuni  ya Kanisa, ambayo ilihusika na kesi za manyanyayaso.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment