Saturday, September 21, 2013

Shambulio la Nairobi lauwa watu kadha

Watu waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
Jengo la maduka liloshambuliwa Nairobi
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.

Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.Inaarifiwa watu watano wamekufa.
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.
Inaarifiwa kuwa watu wengi wamenasa ndani ya jengo.
Magari yaliyoegeshwa nje ya maduka yameharibika
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment