Wednesday, October 9, 2013

‘Kambi za Kujenga Taifa si sehemu ya mateso’

Makuruta wa Jeshi la Kujenga Taifa wakitoa gwaride la heshima katika maadhimisho ya miaka 50 ya JKT. Vijana wengi wanahofia mafunzo haya kwani wanaaamini kambi za jeshi hilo ni sehemu ya tabu na mateso, kitu ambacho JKT imekanusha. PICHA | MAKTABA 
Na Joseph Zablon, Mwananchi
Dar es Salaam. Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), ambazo zimeanza hivi karibuni kwa mujibu wa sheria kwa vijana ambao wamemaliza Kidato cha Nne zimedaiwa kuwa si sehemu ya mateso  bali ni mahsusi kwa ajili ya kuandaa vijana kuwa wazalendo.
Akizungumza na Mwananchi Dar es Salaam jana, Mratibu wa Mafunzo hayo wa JKT, Luteni Kanali Juma Nkhangaa alisema, madai yanayotolewa na baadhi ya watu kuwa ni sehemu ya mateso hayana msingi wowote kwani kila kitu kinafanyika kwa utaratibu.
Alisema ushahidi wa jambo hilo unathibitishwa na baadhi ya wahitimu ambao wakati wanapokaribia kumaliza mafunzo hayo ya miezi mitatu, hutamani kuongezewa muda au wapatiwe ajira katika kambi hizo.
“Sivyo kama inavyovumishwa kwani kila kinachofanyika hapa kinazingatia vigezo vya uwezo wa wahusika,” alisema Nkhangaa na kuongeza kuwa mipango inafanywa ili mafunzo hayo yaweze kuongezwa muda kutoka miezi mitatu ya sasa hadi zaidi.
 Alisema wale ambao wamejiunga na kumaliza mafunzo hayo wamerudi majumbani wakiwa vijana tofauti  na awali na ushahidi wa jambo hilo upo.
Alisema wanao wazazi na walezi wa vijana hao, hivyo amewataka wale ambao wanapata fursa hiyo kwa sasa kuichangamkia fursa hiyo adhimu.
Serikali ilirudisha mpango wa vijana kujiunga na JKT mwaka jana  baada ya mpango huo kusitishwa kunako miaka ya tisini na watu mbalimbali wameishahudhuria mafunzo hayo wakiwamo wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment