Writen by
sadataley
11:48 AM
-
0
Comments
Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameonekana kukwama kufanikiwa kumshawishi Rais wa Marekani Barack Obama kuachana na mpango wake wa kutaka kulegeza vikwazo kwa Iran iliyoonesha utayari wake wa kushirikiana na mataifa mengine kushughulia mpango wake wa nyuklia.
Netanyahu alikutana na Rais Obama kwa mazungumzo ambayo yalijiegemeza kwenye agenda mbili kubwa ambazo ni suala la mpango wa nyuklia wa Iran pamoja na mkakati wa kupata suluhu ya eneo la Mashariki ya Kati kupitia njia ya mazungumzo unaosimamiwa na Marekani.
Rais Obama amemueleza wazi Netanyahu huu si wakati wa kuanza kujadili vitu ambavyo havipo na badala yake inapaswa kutoa muda wa kutosha kwa Serikali ya Iran ambayo imeonesha utayari wake wa kutoa ushirikiano juu ya mpango wake wa nyuklia.
Obama ameweka bayana nchi yake inataka kuona diplomasia ikichukua nafasi yake katika kuhakikisha wanapata suluhu juu ya mpango wa nyuklia wa Iran badala ya kuendelea kulumbana na kupoteza muda zaidi.
Marekani imeanza kuonesha imani yake kwa Rais Mpya wa Iran Hassan Rouhani ambaye amesema Serikali yake ipo tayari kushirikiana na Jumuiya ya Kimataifa katika kufanya uchunguzi juu ya mpango wao wa nyuklia wanaoendelea kuufanya kwa lengo la kuzalisha nishati ya kudumu kwa wananchi wake.
Netanyahu alimueleza Rais Obama ni lazima vikwazo dhidi ya Iran viachwe pale pale hata kama wataonesha utayari wao wa kutoa ushirikiano kwa Jumuiya ya Kimataifa kwa sababu hali hiyo inaweza ikachangia wakakamilisha mpango wao wa nyuklia.
Kiongozi huyo wa serikali ya Israeli amesisitiza vikwazo vya kiuchumi vinapaswa kutolegezwa hata kidogo kwani hivyo ndivyo vimechangia kukwama kwa mpango huo wa nyuklia wa Iran kwani imeshindwa kuwa na pesa za kutosha kuendelea nao.
Waziri Mkuu Netanyahu amesema wao hawana imani kama kweli Iran watakuwa tayari kuachana kabisa na mpango wao wa nyuklia kwani wameshapiga hatua kubwa na wamekuwa katika hatua za mwisho kuzalisha bomu.
Netanyahu baadaye hii leo anatarajiwa kuhutubia Mkutano Mkuu wa Sitini na Nane wa Umoja wa Mataifa UNGA huku wengi wakiendelea kukumbuka mchoro wake aliouonesha mwaka jana juu ya mpango wa nyuklia wa Iran na kueleza hatari ilioyopo kwani Tehran ilikaribia kutengeneza bomu la nyuklia.
Chanzo:http://www.kiswahili.rfi.fr

No comments
Post a Comment