Writen by
sadataley
10:24 AM
-
0
Comments
WAKATI Itafaki ya Umoja wa Fedha Afrika Mashariki inatarajiwa kutiwa saini na wakuu wa nchi mwezi ujao, utekelezaji halisi wa itafaki hiyo utaanza rasmi miaka 10 ijayo. Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayeshughulikia Miundombinu na Mipango,Dk. Enos Bukuku alisema kwamba kipindi hicho cha mpito kitatumika katika kuanzisha taasisi mbalimbali kwa lengo la uangalizi, kuoanisha taratibu na sheria mbalimbali na utekelezaji.Taasisi hizo ni pamoja na Taasisi ya Fedha ya Afrika Mashariki itakayoundwa katika miaka miwili ijayo baada ya kutiwa saini itifaki ya fedha na hatimaye taasisi hiyo kufikia hatua ya kuwa Benki ya Afrika Mashariki.
Uanzishwaji wa taasisi na uoanishaji wa viwango mbalimbali utatoa nafasi ya hatimaye kuanzishwa sarafu moja ifikapo mwaka 2024, Dk. Bukuku alisema.
Taasisi nyingine ya kanda itakayohusika na takwimu pia itaanzishwa.
Dk. Bukuku alikuwa akizungumza na waaandishi wa habari jijini Nairobi, Kenya.
Mkutano huo uliandaliwa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) ambao pia unakwenda sambamba na maonyesha ya kimataifa ya biashara ya Nairobi.
Mkutano huo umewashirikisha viongozi wa biashara, maofisa kutoka sekretarieti ya EAC na maofisa wa serikali ya Kenya.
Akitoa hotuba ya ufunguzi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya, Phyllis Kandie alisema licha ya kupatikana maendeelo kiasi fulani katika mtangamano wa Afrika Mashariki, bado zipo changamoto kadhaa ambazo hazina budi kushughulikiwa ili kusonga mbele zaidi.
Chanzo:http://www.mtanzania.co.tz
No comments
Post a Comment