Writen by
sadataley
9:31 AM
-
0
Comments
Msafara wa misaada kutoka Urusi
Mataifa ya Magharibi yameshtumu
kwa hasira kuingia kwa msafara wa malori ya misaada kutoka Urusi katika
eneo linalodhibitiwa na waasi mashariki mwa Ukraine.
Marekani na Ujerumani zimetaja kitendo hicho
kama hatari na kwamba kuna hofu huenda Urusi ikatumia hatua hiyo kama
sababu ya kuivamia Ukraine.Awali NATO ilikuwa imesema kuwa Urusi inasafirisha silaha kali kuingia nchini Ukraine na kwamba imekuwa ikitumia mizinga yake ndani ya ardhi ya Ukraine dhidi ya vikosi vya Ukraine.
Hatahivyo Urusi inasema kuwa msafara huo umebeba maje-nereta, chakula na maji,lakini waandishi walioona malori hayo wanasema kuwa yamebeba mizigo nusu na kwamba Ukraine inasema kuwa msafara huo unatumiwa kuwasaidia waasi wanaounga mkono Urusi katika eneo la mashariki.
No comments
Post a Comment