Writen by
sadataley
1:47 PM
-
0
Comments
Mechi
Mchezaji mmoja wa soka raia
wa Cameroon amefariki baada ya kupigwa na kitu katika kichwa chake
kilichorushwa kutoka kwa mashabiki mwishoni mwa mechi katika ligi ya
Algeria.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 Albert
Ebosse aliyekuwa akiichezea kilabu kubwa ya JS Kabylie alikuwa
ameifungia timu yake bao la pekee katika mechi ambayo timu hiyo
ilishindwa kwa mabao mawili kwa moja na kilabu ya USM Alger.Kitu kilichomgonga kichwani kilirushwa baada ya mechi kukamilika,wakati ambapo wachezaji walikuwa wanarudi katika chumba cha kujianda.
Waziri wa maswala ya ndani nchini Algeria ameagiza kuanzishwa uchunguzi kuhusu mauaji hayo.
No comments
Post a Comment