Writen by
sadataley
5:17 PM
-
0
Comments
Rais wa Ufaransa Francois Hollande alipokutana na rais wa
Marekani Barrack Obama.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa taifa lake
litawahami wapiganaji WaKurdi iliwakabiliane na wapiganaji wa Islamic State
kaskazini mwa Iraq.
Kulingana na taarifa katika vyombo vya habari vya Ufaransa ,Rais Hollande
amepata ruhusa kutoka kwa mamlaka nchini Iraq kuendelea mbele na mpango huo
mahsusi wa kuidhibiti Islamic State.Mapigano hayo yamesababisha kutokea kwa maelfu ya wakimbizi katika maeneo hayo Kaskazini mwa Iraq.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa atawahami
wakurdi Iraq
Hatua hiyo ya bwana Hollande inafwatia ombi la wakuu wa jimbo la Kurdistan la kuitisha msaada wa kijeshi.
Mapema leo serikali ya Marekani ilituma washauri 130 wa kijeshi katika jimbo la Kurdistan.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa atawahami
wakurdi Iraq
Marekani tayari inaendelea na kampeini ya vita vya hewani dhidi ya IS katika jitihada za kuwazuia wasitawale eneo zima la Kaskazini mwa Iraq.
Kiongozi wa waKurudi Massoud Barzani, ameomba msaada wa kijeshi baada ya Islamic state kutwaa miji kadhaa karibu na jimbo la Kurdistan
No comments
Post a Comment