Writen by
sadataley
10:31 AM
-
0
Comments
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wananchi hivi karibuni
Na Habel Chidawali, MwananchiMpwapwa. Rais Jakaya Kikwete amesema zaidi ya asilimia 80 ya
ahadi alizotoa wakati anaingia madarakani zimetimizwa na zilizobakia
atazimaliza kabla ya kuondoka madarakani.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo juzi katika Kijiji
cha Gulwe, Mpwapwa mkoani Dodoma, alipokwenda kuweka jiwe la msingi la
ujenzi wa daraja.
Alisema wakati anaingia madarakani mwaka 2005,
alitoa ahadi mbalimbali katika maeneo tofauti zikiwamo zilizoandikwa
katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ambazo zimeendelea kutimizwa
kwa kadiri ya upatikanaji wa fedha.
“Sasa tumefikia asilimia 80 ya utekelezaji wa
ahadi zetu, naamini tunaweza kufanikiwa kwa zote na kama tutashindwa
basi tutaacha kidogo sana, lakini kumbukeni tumetekeleza hata yale
ambayo hayakuwa katika ahadi,” alisema Rais Kikwete.
Akizungumzia daraja hilo la Gulwe, aliwaagiza
makandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili likamilike kama
ilivyopangwa.Alisema wananchi wanataka kuona kazi hiyo inakwisha.
No comments
Post a Comment