Tuesday, July 21, 2015

Bulaya kama Lembeli

Hali imeendelea kuwa tete ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum CCM mkoa wa Mara, Ester Bulaya, kutangaza kukitosa kwa kutangaza uamuzi wake wa kutogombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho. Bulaya ambaye alikuwa mbunge machachari kabla ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuvunjwa na Rais Jakaya Kikwete, hivi karibuni , ametangaza kutogombea ubunge kupitia CCM wakati akizungumza na NIPASHE baada ya kazi ya kuchukua fomu ndani ya chama hicho na kurejesha kuhitimishwa rasmi nchini jana. Tangu mwanzo mwa mwaka huu, Bulaya alitangaza kugombea ubunge katika Jimbo la Bunda kupambana na Mbunge aliyemaliza muda wake ambaye ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira. Bulaya amekuwa kada wa pili ambaye alikuwa mbunge kutangaza kutogombea ubunge kwa tiketi ya CCM, mbunge wa kwanza kutangaza kutogombea ubunge kupitia CCM baada ya James Lembeli, ambaye alikuwa Mbunge wa Kahama. Hata hivyo, Bulaya hakuweka wazi kama ana mpango wa kuhamia chama kingine cha siasa na kutimiza azma yake ya kuwania ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Ingawa Bulaya hajaweka wazi, vyama ambavyo vimekuwa vikitajwa kusubiri makada kutoka CCM kujiunga navyo ili wawanie ubunge ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (CUF). Imenukuliwa kutoka NIPASHE
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment