Writen by
sadataley
7:22 AM
-
0
Comments
Rais Jakaya Kikwete amekabidhiwa joho na cheti cha Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Sheria kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Rais Kikwete alitunukiwa shahada hiyo katika mahafali ya 41 ya UDSM yaliyofanyika Oktoba, mwaka 2011 na jana katika chuo hicho.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ilieleza kuwa alitunukiwa shahada hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam kutokana na utumishi wake uliotukuka kwa umma wa Watanzania na jamii nyingine zilizo nje ya mipaka ya Tanzania.
Akisoma maelezo mafupi kabla ya kumkabidhi cheti na kumvisha Joho, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo –Taaluma, Prof. Florens Luoga, alisema Shahada hiyo ya juu miongoni mwa tuzo zinazotolewa na UDSM.
Alisema uamuzi huo ulifanywa na Seneti na kuridhiwa na Baraza la Chuo.
“Seneti ilizingatia busara, wema na umakini uliodhihirika katika maisha yako yote ya uongozi, tangu ulipokuwa kijana hadi ulipofikia ngazi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu, ”alisema.
Rais Kikwete alishukuru kwa shahada hiyo na kueleza nia yake ya kuendelea kukisaidia Chuo Kikuu hicho ambacho ndiyo chuo Kikuu kikongwe nchini.
“Nitaendelea kutoa mchango wangu katika chuo chetu ambacho ndiyo kikubwa hapa nchini kwa lolote ambalo naweza kulifanya kwa ajili ya chuo sasa na hata baadaye,” alisema.
Rais aliahidi na kupata maelezo kutoka kwa Makamu wa Mkuu wa Chuo, Prof. Rwekaza Mukandala ya jinsi mchango wake ulivyochangia katika kutengeneza dira ya UDSM.
Prof. Mukandala alisema baadhi ya mchango mkubwa wa Rais katika chuo hicho ni kuanzishwa kwa shule ya madaktari na masomo ya sayansi ya kilimo Oktoba mwaka huu.
Katika hatua nyingine, Rais Kikwete pia alipokea hundi yake ya Bima ya maisha ambayo amekuwa nayo kwa kipindi cha miaka tisa.
Akimkabidhi hundi hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima Tanzania Limited (NIC), Sam Kamanga alisema uwepo wa Rais kama mteja wa NIC kumesaidia kukuza uelewa na shughuli za shirika hilo.
“Kitendo cha Serikali kukatia bima mali zake na taasisi zake, kumeongeza uwezo wa kifedha wa shirika na soko la bima,” alisema na kuwataka watu binafsi, taasisi mbalimbali na mashirika ya kiserikali kukata bima kwa ajili ya maendeleo na akiba ya baadaye.
Rais Kikwete alilitaka NIC kuongeza juhudi katika kuhamasisha na kuelimisha Watanzania umuhimu na manufaa yanayopatikana kutokana na bima.
Chanzo:Ipp Media
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
No comments
Post a Comment