Thursday, July 23, 2015

Usajili wa kielektroniki Tanzania umeanza

Usajili wa kielektroniki Tanzania umeanza Leo imeingia siku ya pili kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kujiandikisha katika daftari la kupiga kura kwa kutumia mfumo wa kieletroniki maarufu kama BVR. Wakazi wapatao milioni tano ambao wana sifa ya kupiga kura wanalengwa Katika zoezi hili ambalo linatarajiwa kudumu kwa siku kumi, tume ya uchaguzi ya taifa inatarajia kusajili wakazi wapatao milioni tano ambao wana sifa ya kupiga kura. Zoezi hili linatarajiwa kudumu kwa siku kumi Hata hivyo, wakati zoezi hilo likiendelea, tayari linaonekana kuwa kero miongoni mwa wakazi. Vituo vingi vinadaiwa kucheleweshwa Katika baadhi ya vituo ambao inaarifiwa kuwepo kwa ucheleweshwaji huku katika maeneo mengine kukiwa na mashine chache za uandikishaji. Mashine zinadaiwa kuwa chache Je umejiandikisha kupiga kura katika mfumo huo mpya wa kielektroniki? Tusimulie yaliyokusibu Chanzo: BBC Swahili
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment