Writen by
sadataley
2:37 PM
-
0
Comments
WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa,
amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya Sumitomo Mitsui anayejenga
barabara ya juu (fly over) ya Tazara, kuongeza kasi ya ujenzi huo.
Prof. Mbarawa alitoa agizo hilo jijini Dar es Salaam juzi muda mfupi
baada ya kumaliza kutembelea mradi huo uliozinduliwa Desemba mosi, mwaka
juzi na kufurahishwa na kasi ya ujenzi inayoendelea.
Ziara hiyo aliifanya akiwa amefuatana na Balozi wa China nchini Tanzania, Masaharu Yoshida.
Licha ya kupongeza hatua ya ujenzi ilipofikia hivi sasa ya kukamilika
kwa asilimia 25.3 kati ya 25.8, alimtaka mkandarasi huyo kuongeza kasi
zaidi ya ujenzi huku akizingatia ubora na viwango vilivyowekwa.
“Kama mnakumbuka, Rais John Magufuli wakati akizindua mradi huu aliomba
muda wa ujenzi ambao ni miezi 35, angalau upungue, nimefurahishwa na
kasi yenu hakikisheni miezi ya ujenzi wa mradi inapungua zaidi ili
kuwawezesha wananchi na wadau wengine kunufaika na fursa hii
itakapokamilika, ”alisisitiza Mbarawa.
Pia alimtaka mkandarasi kuhakikisha ujenzi huo unatekelezwa kwa viwango
vilivyowekwa ili viendane na fedha ambazo ni zaidi ya Sh. bilioni 96.5
zilizotengwa kutekeleza mradi huo unaotarajiwa kukamilika Oktoba,
mwakani.
Aidha, aliwataka wafanyakazi wote katika mradi huo kufanya kazi kwa
bidii na uaminifu kwa kuwa serikali ina mpango mwingine wa kujenga
fly-over kama hiyo itakayowawezesha kupata fursa ya ajira.
Naye Balozi Yoshida alimhakikisha Waziri Mbarawa kuwa ujenzi wa mradi
huo utamalizika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa na hivyo
kuondoa changamoto ya msongamano katika barabara ya Nyerere na Mandela.
Mkurugenzi wa Miradi kutoka Wakala wa Barabara nchini (Tanroads),
Mhandisi Chrispianus Ako, alisema kati ya nguzo 66 zinazohitajika kwenye
awamu ya kwanza ya ujenzi huo, tayari 43 zimeshasimikwa ardhini, hali
itayoufanya ujenzi huo kwenda kwa kasi.
Alisema kazi ambazo zimefanyika kutoka Septemba 30, mwaka jana hadi jana
ni ujenzi wa barabara ya Kusini mwa mradi huo, ambayo ikikamilika
itatumiwa na magari ili ujenzi wa daraja hilo uendelee.
“Mheshimiwa Waziri Mbarawa, kutoka Septemba, mwaka jana ulivyotembelea
mradi na kukuta maendeleo ya ujenzi ambayo yalikuwa kwa asilimia 13, kwa
sasa tumepiga hatua nyingine na ujenzi wa mradi kwa awamu hii umefikia
asilimia 25,” alisema.
Alisema kutoka wakati huo kazi ambazo zilikuwa zikifanyika ni ujenzi wa barabara upande wa Kusini, kusafisha eneo la mradi,
kujenga tabaka la kwanza ambapo hadi sasa tayari kumeshawekwa lami.
Alisema kazi iliyobaki ni kuweka tabaka la pili juu.
Pia alisema katika ujenzi wa daraja, wameanza kusimika nguzo zinazoanzia mita tisa hadi 13.
Chanzo: Muungwanablog

No comments
Post a Comment