Writen by
sadataley
2:08 PM
-
0
Comments
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra
(kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa
kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker .
JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab
wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila
kufungua kifua (Catheterization).
Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra
(kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa
betri ambalo litatumiwa na kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa
jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa
kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali
za matibabu ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Daktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuhudumia Monica Mahenge
ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo baada ya kufanyiwa matibabu ya moyo
kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua (Catheterization) kwa
kutumia mtambo wa Cath lab . Monica ni mmoja kati ya wagonjwa 16 ambao
JKCI kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya BLK ya nchini
India walitoa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve),
balloon mitral valve procedure (Valvuloplasty), kuzibua mishipa ya damu
ya moyo, kufunga kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme (Pacemaker)
na kuangalia utendaji kazi wa Moyo.
Madaktari bingwa wa Moyo, Wauguzi,
Technologists, wataalam wa dawa za usingizi wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kumaliza kumpatia mgonjwa huduma za matibabu ya
kuzibua milango ya moyo (Valve) bila kufungua kifua (Catheterization)
kwa kutumia mtambo wa Cath lab .
Kazi ya kutoa huduma ya matibabu ya Moyo
kwa mgonjwa kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua
(Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab ikiendelea.
Picha na Anna Nkinda – JKCI
No comments
Post a Comment