Writen by
sadataley
11:50 AM
-
0
Comments
Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn
Mkutano wa IGAD umefunguliwa rasmi jumamosi jijini Narobi ambapo wito
umetolewa na viongozi wa nchi wanachama wa shirika hilo kufanya kila
wawezalo kuhakikisha kuwa wakimbizi wanapewa hifadhi bila kujali nchi
wanazotoka.
Waziri mkuu wa Ethiopia, Hailemariam
Dusalegn alisisitiza wanachama kuwa wakimbizi lazima wahifadhiwe kwa
vyovyote vile Kulingana na sheria za kulinda wakimbizi za kimataifa.
Hadi sasa raia wa Somalia wapatao Milioni mbili wameyakimbia makwao huku wengi wakiishi nchini Kenya, Ethiopia na nchini Uganda.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukitoa wito kwa nchi za hasa Kenya kuendelea kuwapa hifadhi wakimbizi wa Somalia.
No comments
Post a Comment