Writen by
sadataley
8:57 AM
-
0
Comments

RAIS wa Serikali ya Awamu ya Nne, Dk
Jakaya Kikwete kesho anatarajiwa kuzindua Taasisi ya Maendeleo ya Jakaya
Mrisho Kikwete (JMKF) .
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na taasisi hiyo, uzinduzi huo utafanyika katika Hoteli ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na baada ya uzinduzi huo, Dk. Kikwete ataendesha kikao cha kwanza cha bodi ya taasisi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na taasisi hiyo, uzinduzi huo utafanyika katika Hoteli ya Hyatt Kempinsk The Kilimanjaro jijini Dar es Salaam na baada ya uzinduzi huo, Dk. Kikwete ataendesha kikao cha kwanza cha bodi ya taasisi hiyo.
Taasisi hiyo imeundwa ili kusaidia
Tanzania na Afrika katika kuimarisha amani, afya, utawala bora na
maendeleo endelevu.Aidha taasisi hiyo itajikita katika maendeleo
endelevu kwa kusaidiana na wadau wengine kukabiliana na umasikini,
kusaidia mkulima mdogo, kulinda mazingira na kukabiliana na athari za
tabianchi.
Taasisi hiyo itasaidia pia katika afya
ya mama na mtoto, kukabiliana na ugonjwa wa malaria na kuboresha lishe
ya wananchi.Katika elimu, itaboresha elimu katika kuwasaidia
wajasiriamali kwa mafunzo na pia itasaidia katika utawala bora na
utafutaji amani.
Taasisi hiyo imesajiliwa na itakuwa
chini ya uongozi wa bodi ya wadhamini wa kimataifa yenye wajumbe kutoka
ndani na nje ya Tanzania ikiwemo Guinea Bissau na Marekani.
Wajumbe kutoka Tanzania ni aliyekuwa
Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara, Daktari Bingwa wa Upasuaji Profesa
William Mahalu, Balozi Mwanaidi Maajar, Genevive Sangundi na Mkurugenzi
Mtendaji wa kundi la makampuni ya SS Bakhresa, Abubakar Bakhresa.
No comments
Post a Comment