Writen by
sadataley
5:09 PM
-
0
Comments

Kwa siku kadhaa nimekuwa na kazi za nje ya mji wakati mwingine nakosa kujua nini kinaendelea mtandaoni. Ila leo nimepata bahati ya kufuatilia walau kwa muhtasari nini kilikuwa kinaendelea katita mitandao ya kijamii.
Kwa bahati, wakati natembelea mtandao mmoja, ukawa uko mubashara (live) wa zoezi la kuapishwa waheshimiwa mawaziri, mabalozi hali kadhalika Justice Stela Mugsha kuwa Kamishna wa tume ya mahakama.
Mara baada ya zoezi la kuapishwa kuna hotuba kadhaa zikatolewa kwa kifupi. Prof. Kabudi alinukuu kitabu cha zaburi huku balozi Mabumba akimnukuu Mfalme Daud kwa kuomba hekima na busara aweze kujua namna ya kuwakilisha Tanzania nchini Comoro hasa kuiunga Tanzania kwa fursa za nyama na mazao ya kilimo ili Watanzania tuweze kuuza visiwani Comoro.
Mwisho Mheshimiwa Rais Magufuli akazungumza kwa kifupi kuhusu mitandao na uzushi unaofanywa mitandaoni. Kwa mara nyingine tena akatoa rai kwa Watanzania kuandika “ideas” za kutatua matatizo yanayoikumba Tanzania badala ya uzushi wa kuwa Mwakyembe amegoma uteuzi na kuwa kulikuwa na habari Comrade Kinana angelonga na wahabari leo hii.
Nikajua kumbe hata Mheshimiwa huwa anachungulia chungulia walau kujua nini tunaandika. Katikati ya mazungumzo yake, mara akagusia kumtaka Balozi Possi alete fursa za uwekezaji na kutoa rai “pasi zikipigwa”, basi walio serikalini wasikabe bali waunganishe ili magoli ya uwekezaji yaingie.
Mara nikakumbuka, miezi kadhaa, nilikuwa “napiga story” na mtani wangu anaitwa Chilo wa kabila la kigogo. Mimi ni msukuma na kiasili wagogo ni watani wa wasukuma. Mtani wangu Chilo alinipa wazo biashara ambalo linaweza kuwa sehemu ya kuijenga Tanzania ya viwanda. Wakati tunadadavua akatania; ugumu ni namna gani mawazo yake na y a Watanzania wengine kama yeye yanaweza kutafsiriwa na wasomi hususani wafanya maamuzi serikalini ili Tanzania isonge mbele.
Niliposikiza mpango biashara wa mtani wangu Chilo, alikuwa na suluhisho la kutengeneza ajira walau 15 na biashara yake kulipa kwa uchache kodi ya ongezeko la thamani walau milioni 700 ikiwa ni pamoja ya kuwaingiza hao wafanyakazi wengi kwenye mifumo ya bima ya afya hali kadhalika mifumo ya mifuko ya hifadhi ya jamii.
Mie nikampa dongo kwa kumnukuu Robert Kiyosaki kwa kumwambia “You have to be smart. The easy days are over.” (Unatakiwa kuwa smart maana siku za nibebe nibembeleze zimeisha). Leo hii, Chilo akanitumia barua pepe kwa kunipa dongo kuwa tumtanie Ngosha mwezio (akiwa na maana mwanaume mwenzangu) ambae ni Rais Magufuli. Chilo akasema, tumtanie mkuu wa kaya japo hapendi utani na hajaribiwi kwa kumpa andiko la kutengeneza ajira ya vijana 15 kihalali ikiwa ni pamoja na kuwa wadau wa kulijenga taifa kwa kulipa kodi kutokana na mapato ya biashara ya Chilo.
Binafsi nikamtania Chilo kuwa, ukiandika, umpigie simu “flani” akusaidie kuipiga pasi andiko lako maana ni suluhisho kwa ajira na “Ngosha” ataka ideas za kiamaendeleo. Chilo akijiuliza, je huyo tunaempa, atafikisha au atakaba “penati” au ataiba wazo la mradi? Ahh kila mmoja akakosa jibu.
Nikamwambia Chilo kwa kuwa andiko unalo, kumbuka simulizi za kale enzi za biblia. Ukiogopa kwenda nchi ya asali na maziwa waliko maadui unaweza kufa na njaa. Bora uende nchi ya washami hata kama kuna majamaa wanatisha ila kuna chakula na maziwa. Chilo akasema, angeweza, angetumia akili ya kama yule mkulima wa tumbaku alietoka Tabora mpaka Geita na kupiga kelele mpaka Rais Magufuli akamsikia na akampa ahadi ya msaada.
Kwa kuwa mara kadhaa Rais amekuwa akinadi uzalendo, huenda vijana waliomzukunguka nao ni wazalendo na watafikisha andiko ili wali-digest kuona kama ni wazo kweli la kutatua moja ya tatizo hali kadhalika kuleta ajira.
Baadae Chilo akataka kuandika wazo lake mtandaoni akitegemea mkuu wa kaya atasoma. Nikamwambia ukiandika tu, litaibiwa maana litakuwa halina patent(hati miliki) mpaka ukasajili patent panapohusika. Mwishoni mie nikwambia Chilo, weka andiko lako vizuri na tulitume kwa njia ya posta, huenda likasomwa na vijana wa mkuu wa kaya na baadae ukamtafuta ukamwage ujuzi ili uwe sehemu ya ajira na kutoa huduma yenye kuchangia kodi pia kwa maendeleo ya Taifa.
Tumeachana na Chilo jioni hii, tukijiuliza, tuandike wapi ili Rais asome. Maana kuna woga wa kuibiwa wazo au wasaidizi kupuuza wazo lake la kibiashara la kutoa huduma yenye kutengeneza fedha.
Mwishoni nikawaza tu, mbona mambo mabaya yakiandikwa, wahusika hutafutwa kwa haraka sana na kupelekwa kwa palate kushtakiwa? Je mawazo mazuri ya kutatua matatizo yanafanyiwa kazi kwa kasi sawia na kuwadhibiti mawazo mabaya?
Bado tunafikiria na mtani wangu ni kwa namna gani tuandike wazo la Kibiashara ili kama mfalme Farao alivyopata msaada wa suluhisho la kukusanya chakula Misri toka kwa “Mfungwa Yusuf” Mungu amsaidie mtani wangu Chilo ambae pia ni mtani wa Rais Magufuli pia, andiko lake la biashara ya huduma ya ajira kwa vijana 15 na biashara yake ikifanikiwa, basi aweze kuwa sehemu ya kulipa kodi ya walau milioni 700 kwa mwaka.
Binafsi namtakia kila la heri mtani wangu Chilo ili daraja kama ambalo alilipata Yusuf kutambulishwa kwa Farao, basi nae atambulishwe kwa Rais Magufuli. Ni imani yangu pia tabia za wanaokaba penati wataruhusu magoli yafungwe ili Chilo aweze kufunga goli.
Mie ninaendika waraka huu kwa niaba ya Chilo, nina imani kubwa ningeandika jambo baya, kabla nusu saa haijaisha, ningewajibika kwa “upuuzi” ambao ningekuwa nimeuandika. Ila ujumbe huu ukipata “laverage” kumfikia Ngosha ambae pia ni mtani wa Chilo, huenda kama jinsi ambavyo Rais Magufuli alikubali kumsikiza mkulima wa tumbaku na kuwa sehemu ya suluhisho. Mtani wangu Chilo, mtani wako Ngosha akikusiliza na ukawa sehemu ya mchango wa kuijenga Tanzania mpya, kumbuka kumshukuru ikiwezekana “publicly” kama wale wakoma wa enzi za Yesu wa Nazareth ili nasi tujifunze kwa wazo lako la kibiashara.
Cha mwisho, nina imani kuwa human asset ambae ni mtani wangu Chilo, akisikizwa na business plan yake ikafanyiwa kazi, itanikumbusha ukweli wa maneno ya mmoja wa Mwl. Shloma Sasson alienifundisha kilimo-biashara pale Galilee International Management Institute kuwa “the best success can be obtained in African Countries when decision makers will be able to harness solutions from their people’s brains”…. (Mafanikio bora katika nchi za Kiafrika yatapatikana pale wafanya maamuzi watakapoweza kuvuna suluhisho la matatizo kutoka kwa akili za watu wao wenyewe). Mwl. Shlomo alitusimlia kidogo kumbukumbu za Mfalme Sauli kumpa nafasi kijana mdogo Daudi kwa kumpa nafasi ya kupigana na Goliath kwa kuwa ni yeye pekee alieonekana alikuwa na ujasiri wa kweli kumuua Goliath.
Cha mwisho, nina imani kuwa human asset ambae ni mtani wangu Chilo, akisikizwa na business plan yake ikafanyiwa kazi, itanikumbusha ukweli wa maneno ya mmoja wa Mwl. Shloma Sasson alienifundisha kilimo-biashara pale Galilee International Management Institute kuwa “the best success can be obtained in African Countries when decision makers will be able to harness solutions from their people’s brains”…. (Mafanikio bora katika nchi za Kiafrika yatapatikana pale wafanya maamuzi watakapoweza kuvuna suluhisho la matatizo kutoka kwa akili za watu wao wenyewe). Mwl. Shlomo alitusimlia kidogo kumbukumbu za Mfalme Sauli kumpa nafasi kijana mdogo Daudi kwa kumpa nafasi ya kupigana na Goliath kwa kuwa ni yeye pekee alieonekana alikuwa na ujasiri wa kweli kumuua Goliath.
Kwa kuwa mheshimiwa Rais Magufuli huwa anatembelea mtandao pia, nina imani atamtafuta mtani wangu ambae pia ni mtani wake. Ikitokea basi Rais asiweze kuiona makala hii ya “kumnadi” Chilo na watu wenye mawazo kama yake; ninatumai wasaidizi wazalendo wa “Bwana Mkubwa” wataweza kumpigia pasi mtani wangu Chilo ili asikike.
Dr. A. R. Bernard aliwahi kusema “thoughts have power, thoughts have potential, thoughts can be our success or failure”… Mawazo yana nguvu, mawazo yana uweza uliotulia na yanaweza kutoa mafanikio ua kufeli… Hivyo basi ili matokeo yatokee ni pale wafanya maamuzi watamsikiza Chilo na watu wa aina ya Chilo. Wakipewa nafasi ya kutoa mawazo yao kutoka hali ya kuwa “potential” (hali ya kuwa hapo hapo yalipo) na yawe dynamic (yawe kwenye mwendo kwa kufanyiwa kazi).
Ninamsifu Rais Mafufuli kwa kuamua wakati flani kujenga barabara ya hapa Mwanza kutoka Mission kuelekea Airport kama alivyotaka barabara ya Morroco jijini Dar es Salaam ifanyiwe kazi. Alipoamua, it was a potential idea to kinetic action. (ilikiwa ni wazo lililokuwa limetulia likafanyiwa kazi na sasa miundombinu inajengeka). Kumbe ni suala la kuamua hasa katika mambo mema yenye tija. Na uamuzi ukifanyika kwa wakati inamweka Chilo mwenye wazo (potential idea), kuvunwa wazo lake kwa kushirikiana na wafanya maamuzi na lifanyiwe kazi. Na yawezekana kabisa ajira alizopanga na utoaji huduma ukawezekana ili pia awe sehemu ya mlipa kodi kwa maendeleo ya Taifa hili.
Kwa pamoja tunajukumu la kuijenga nchi yetu Tanzania. Tukishirikiana, mwendo kasi utakuwa mkubwa kufikia malengo.
Fredrick Matuja
fmatuja@hotmail.com
fmatuja@hotmail.com
No comments
Post a Comment