Writen by
sadataley
2:46 PM
-
0
Comments
Wanachama na mashabiki wa nga jijini Mwanza wamemtaka kocha George
Lwandamina kuondoka na mabegi yake wakati timu hiyo itapokwenda Zambia
kurudiana na Zanaco wiki ijayo.
Yanga itacheza mechi yake ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi
ya Zanaco ugenini Jumamosi ijayo ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa
sare 1-1 na Wazambia hao Jumamosi iliyopita.
Wanachama hao, Emmanuel Majura “Emma Yanga” na Mzamiru Abeid walisema
kuwa kutokana na matokeo mabovu wanayoyapata wao wanachama ndio
wanaoumia zaidi na kusisitiza kocha huyo aondoke.
Walisema akiondoka ni bora aende na mabegi yake na asirudi kwani hawajaona kipya walichokifanya tangu akabidhiwe timu hiyo.
Majura alisema kuwa kocha huyo ameanza kuwapotezea hata matumaini ya
kutetea ubingwa wa Ligi Kuu kutokana na kushindwa kupanga vizuri hata
kikosi.
“Kocha huyu (Lwandamina) bora aondoke tena haraka hajatufanyia lolote
tangu afike hapa, tumeshuhudia timu inacheza chini ya kiwango na
kusababisha sisi wanachama kuumia tu,” alisema Majura.
Kauli hiyo iliungwa mkono na Abeid ambaye alisema Lwandamina hajaleta
mabadiliko yoyote kama walivyotarajia na kushauri arejeshwe kikosini
Hans Pluijm.
“Naunga mkono kuondoka kwa Lwandamina, tena bahati nzuri Yanga inaelekea
huko kwao (Zambia) bora akusanye mabegi yake aondoke nayo,” alisema
Abeid.
Katibu wa Yanga tawi la Mwanza, Khamis Maluli na alisema kuwa kocha huyo apewe muda hadi ligi iishe.
Alisema kuwa suala la matokeo kuwa mabovu ni hali ya mpira na kwamba bado ni mapema kwa Mzambia huyo kulaumiwa.
“Apewe muda tu, aangaliwe kama Arsenal kocha wao (Arsene Wenger),
amedumu kwa muda gani na matokeo gani amepata sasa hivi? Tumpe muda
Lwandamina,” alisema Maluli.

No comments
Post a Comment