Writen by
sadataley
1:36 PM
-
0
Comments
Rais Dkt John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Machi,
2017 ameongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika
Chamwino Mkoani Dodoma. Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman
Kinana akizungumza jambo wakati wa kikao cha Usalama na Maadili
kilichoongozwa na Rais Dkt Magufuli,Chamwino mkoani Dodoma.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein mapema leo,Chamwino mkoani Dodoma,pichani kati ni Makamu wa Rais
Mama Samia Suluhu Hassan

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza jambo na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein mapema leo,Chamwino mkoani Dodoma.
Chanzo:Mjengwa Blog

No comments
Post a Comment