Writen by
sadataley
4:48 PM
-
0
Comments
Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo amekutana na kufanya mazungumzo
na washirika wa Maendeleo kutoka nchini Uingereza (DFID) ambapo Kwa
pamoja wamekubaliana kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili
ikiwa ni pamoja na kuboresha Miundombinu katika sekta ya Elimu.
Waziri Ndalichako amefanya
mazungumzo hayo mjini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine waziri
amesisitizia zaidi suala la kuboreshwa Kwa mazingira ya kujifunzia Kwa
wanafunzi wenye mahitaji maalumu, kusisistiza kuwa eneo hilo
linahitaji kuwekewa Nguvu zaidi.
Waziri amewaeleza washirika
hao wa maendeleo kuwa zipo changamoto katika shule za wanafunzi wenye
mahitaji maalumu, hivyo ili kuwawezesha wanafunzi hao lazima miundombinu
iwe rafiki ambayo itawasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.
Waziri pia amezungumzia suala
la ujenzi wa mabweni kwa wanafunzi wa kike, hususan kwa wale wanaoishi
vijijini.Amesema wanafunzi wa kike wanapata changamoto ya mimba za
utotoni kutoka na baadhi ya shule kukosa mabweni na hivyo wanafunzi hao
wakike kuingia kwenye vishawishi.
Pamoja na mambo mengine
waziri Ndalichako pia ameelezea baadhi ya changamoto ya kuwepo Kwa Elimu
bila malipo kuwa ni pamoja na uhaba wa vyumba vya madarasa, uhaba wa
matundu ya vyoo, uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi.
No comments
Post a Comment