Writen by
sadataley
4:01 PM
-
0
Comments

Mkutano wa 39 wa shirikisho la soka barani Afrika CAF leo March 16 2017 ulikuwa unafanyika Addis-Ababa Ethiopia, mkutano huo ambao ulijadili mambo kadhaa ikiwemo kusikiliza ombi la Zanzibar la kutaka kuwa mwanachama rasmi wa CAF, ulifanyika pia uchaguzi wa Rais wa shirikisho hilo.

Ahmad Ahmad
Wagombea wa nafasi za Urais walikuwa ni Rais wa sasa wa shikisho hilo Issa Hayatouna Ahmad Ahmad wa Madagascar, katika uchaguzi huo uliyofanyika leo Ahmad Ahmadamemshinda Issa Hayatou kwa kura 34 wakati Hayatou akiambulia kura 20.

Issa Hayatou
Hayatou anaondoka madarakani baada ya kutawala shirikisho la soka barani Afrika CAFkwa miaka 27, Issa Hayatou aliingia madarakani mwaka 1988 na ndio Rais wa CAFaliyetawala muda mrefu zaidi akifuatiwa na Yidnekatchew Tessema aliyetawala miaka 15.
Waliyowahi kuwa Marais wa CAF
- Abdel Aziz Abdallah Salem (1957-1958)
- Abdel Aziz Moustafa (1958-1968)
- Abdel Halim Muhammad (1968-1972)
- Yidnekatchew Tessema (1972-1987)
- Abdel Halim Muhammad (1987-1988)
- Issa Hayatou (1988-2017)
- Ahmad Ahmad (2017-)
Chanzo:Millardayo.com
No comments
Post a Comment