Saturday, March 11, 2017

RATIBA MPYA YA SERENGETI BOYS YATOLEWA


SERENGETI-BOYS-SA
Wakati Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) likirejesha nyuma kwa wiki moja, timu ya taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys inatarajiwa kuanza kambi mpya Machi 12, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Serengeti Boys itakuwa kambini Dar es Salaam hadi Machi 26, mwaka huu ambako itakwenda Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mechi za kirafiki za kimataifa kujiandaa na michuano ya Afrika ambayo sasa itaanza Mei 14, 2017 badala ya Mei 21, mwaka huu.
Michezo ya kirafiki ya kimataifa itakuwa ni dhidi ya timu za vijana za Rwanda (Machi 28, 2017), Burundi (Machi 30, mwaka huu) na Uganda Aprili 2, mwaka huu). Michezo yote itafanyika Uwanjawa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera.
Sababu za kuwa na  mechi hizo Bukoba ni kupunguza gharama kwa TFF kwani ni rahisi kusafirisha timu hizo kutoka nchi jirani za Rwanda, Burundi na Uganda.
Timu hiyo itarejea tena Dar es Salaam Aprili3, mwaka huu ambako siku inayofuata itaagwa kwa kupewa bendera na mmoja wav iongozi wa nchi kabla ya kusafiri Aprili 5, mwaka huu kwenda Morocco kwa ajili ya kambi.
Timu hiyo itaunganisha kwenda Cameroon Mei mosi, mwaka huu ambako Mei 3, 2017 itacheza mechi ya kwanza na Cameroon kabla ya kurudiana Mei 6, mwaka huu na siku inayofuataita kwenda Gabon.
Serengeti Boys n itimu yav ijana ambayo imefuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Gabon kuanzia Mei 14, mwaka huu. Timu hiyo imepangwa Kundi ‘B’ pamoja na mabingwa watetezi Mali, Niger na Angola. na ina lengo ya kurejea na Kombe la Afrika kwa vijana.
Lakini ikitokea imekosa nafasi hiyo angalau ikafika nusu fainali ambako kwa mafanikio hayo itakuwa tayarii na tiketi mkononi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia huko India, Novemba, mwaka huu.
Chanzo:Mjengwa Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment