Writen by
sadataley
11:56 AM
-
0
Comments
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia na
Kamanda wa jeshi la taifa la Libya wamefanya mazungumzo kuhusu
kuendeleza ushirikiano wa kijeshi kati ya pande mbili.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia
imeripoti kuwa, Michail Bogdanov Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia
amesisitiza katika mazungumzo yake na Khalifa Haftar, kamanda wa jeshi
la taifa la Libya huko Moscow kuhusu msimamo wa Russia katika kuunga
mkono mchakato wa kisiasa nchini Libya.
Viongozi hao wa Libya na Russia
wamebadilishana mawazo kuhusu matukio ya Libya na wakasisitiza kuhusu
umuhimu wa kufanyika mazungumzo mapana kwa kuyashirikisha makundi yote
ya kisiasa na uongozi wa maeneo mbalimbali ili kuiondoa Libya katika
mgogoro wa kisiasa unaoikabili.
Bogdanov ameunga mkono kulindwa umoja wa
wananchi na wa ardhi nzima ya Libya. Wakati huo huo duru za Marekani na
Misri zimearifu kuwa kikosi maalumu cha wanajeshi kimetumwa katika
kambi za kijeshi huko Misri karibu na mpaka na Libya.
No comments
Post a Comment