Writen by
sadataley
10:45 AM
-
0
Comments
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka wa kwanza Kulia Akipeana Mikono na watendaji Mara Baada ya Kuwasili kufungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga, iliyofanyika katika katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akiwasili katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya kufungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.
Mwenyekiti Wa Umoja wa Vijana Wa Chama cha mapinduzi Ndg:Amani Kajuna akizungumza kumkaribisha Ndg:Kaimu katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka kufungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.iyofanyika katika katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
Kaimu Katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka akifungua semina elekezi kwa makatibu wa wilaya na mikoa ya Mbeya, Iringa, Songwe, Katavi, Rukwa, Kigoma, Kagera, Tanga.iyofanyika katika katika ukumbi Wa mikutano CCM Mkoa Wa Mbeya.
Makatibu wakimsikiliza kwa Makakini
Akizungumzia kuhusu mabadiliko ya katiba CCM na kanuni za jumuiya amewahimiza watendaji hao kutopindisha na kupotosha katika eneo lolote badala yake wafanye kazi ya kuelimisha na kusimamia utekelezaji wake.
Amesema mabadiliko ya katiba ya CCM kimsingi yameonyesha njia, mweleko na dira ya chama katika kujimarisha kisiasa.
*”Mabadiliko Katiba ya CCM na kanuni za jumuiya hayakuzuka kama mvua za vuli yamefanyiwa upembuzi yakinifu, tathmini za kitaalam katika taaswira ya sayansi ya siasa, yakitekelezwa kwa kufuata misingi yake, CCM itaendelea kupeta miaka mia mbili ijayo “Alisema*
Akizungumzia kuhusu uchaguzi Wa ndani ya chama na jumuiya alisema. *”Lazima mkumbuke ninyi ndio wakurugenzi wa uchaguzi wa UVCCM katika maeneo yenu msiende kusimamia chaguzi mkiongozwa na utashi na visasi,
fuateni kanuni, taratibu ili kuzifanya chaguzi zetu kuwa huru, za haki na za wazi, nawakumbusha wakati wote pendeni kuishi katika matamshi na maelekezo ya Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt Magufuli “Alisisitiza*
fuateni kanuni, taratibu ili kuzifanya chaguzi zetu kuwa huru, za haki na za wazi, nawakumbusha wakati wote pendeni kuishi katika matamshi na maelekezo ya Mwenyekiti wetu wa CCM Dkt Magufuli “Alisisitiza*
Aliwakumbusha watendaji hao wa jumuiya kuwa watakuwa na jukumu kupitia vikao vyao vya kikatiba na kikanuni kuchuja na kuwapima wagombea kwa vigezo stahili na si kuzoazoa watu ambao hawatokani na jumuiya wala CCM.
Kuhusu Mali za jumuiya alisema UVCCM imeamua kuandaa semina hiyo kuwajengea uwezo watendaji katika masuala ya uchumi na biashara, namna ya kuibua miradi mipya, kuandaa maandiko ya miradi na usimamizi ili iwe endelevu,
namna ya kutumia fursa zilizopo kuweza kuongeza kipato cha jumuiya na kuwatoa katika ombwe la kujiona hawezi kuendesha jumuiya bila kuomba omba.
namna ya kutumia fursa zilizopo kuweza kuongeza kipato cha jumuiya na kuwatoa katika ombwe la kujiona hawezi kuendesha jumuiya bila kuomba omba.
*”Nendeni mkabuni, mkatunze na kulinda Mali za jumuiya ili zinufaishe taasisi hatutamvumilia mbadhirifu au mhujumu wa mali au kutumia mamlaka yake vibaya katika kusimamia mali hizo, hata mimi ikibainika pako pahala nimekiuka taratibu au maelekezo kwa makusudi niko tayari kuwajibika ili kulinda heshima na nidhamu ya Mali zetu tunahitaji kuiona UVCCM mpya si kwa maneno tena bali ni kwa vitendo”*
Kaimu Katibu Mkuu aliwataka vijana wote nchini kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli kwani amekuwa akipigania maslahi ya umma, kujenga uchumi imara, kutetea haki na ujenzi wa demokrasia endelevu .
picha na FAHADI SIRAJI
No comments
Post a Comment