Thursday, March 9, 2017

Simba Ya Tanzania Iliwahi Kufanya Kama Barcelona 1979!


Image result for simba fc in 1979
Ndugu zangu,
Si wengi wenye kukumbuka, hususan wapenzi wa Yanga, kuwa mwaka 1979 Simba ya Tanzania, maarufu kama Wekundu wa Msimbazi, walipata kuthibitishia ulimwengu wa soka kuwa mpira una ' Miujiza yake' baada ya kugeuza matokeo ya kufungwa 4-0 nyumbani na Mufulira Wanderes.
Nilikuwa mdogo sana pale National Stadium niliposhuhudia tukiloweshwa 4-0. Tuliondoka uwanjani tukiwa wenye simanzi kubwa.
Lakini, kwa mpenzi wa Simba, mahali fulani kwenye moyo wake anajua kuwa Simba kamwe hakati tamaa na ana uwezo wa kufanya lolote lile la kushangaza. ( Rejea ya Kichuya na Mavu-goals!)
Ikumbukwe, Simba ina rekodi ya kuwa ya kwanza Tanzania kuingia hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ndio, mwaka ule wa 1979 Simba waliondoka kimyakimya kuelekea Lusaka. Huko Simba wakaweka rekodi na kuandika historia ya kugeuza matokeo ya 4-0 kwa kuifunga Mufulira Wanderers ya Zambia 5-0 pale Lusaka, na mbele ya Rais Kaunda.
Tunawakumbuka wachezaji aina ya George Kulagwa waliofanya makubwa wakiwa na Simba wakati huo.
LAKINI, kubwa zaidi na la kuzingatiwa, ni kuwa Simba ina rekodi ya kuifunga Yanga 6-0 mwaka 1977. Yanga hawajaifikia na kamwe hawataifikia rekodi hiyo.
Subiri waamke, kama wanaweza kupinga hili!
Chanzo: Mjengwa Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment