Writen by
sadataley
1:13 PM
-
0
Comments
![]() |
| Madini ya Tanzanite ambayo yanapatikana eneo la mererani pekee duniani yakiwa tayari yamekatwa na kusanifiwa sasa yatauzwa kimataifa katika kituo kitakachonjengwa Arusha |
![]() |
| Mtaalamu wa kukata madini Adam Idd Lacha akiwa anakata na kusanifu madini ya Tanzanite ya kampuni ya Tanzanite one ambayo ndio inatoa mafunzo hayo. |
![]() |
| Mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Sky Associate Group, Faisal Juma Shahbhai akizungumza na madali wanawake wa madini |
![]() |
|
| Muonekano wa Mgodi wa kisasa wa uchimbaji madini wa tanzanite One Mererani kwa nje |
PICHA ZOTE NA MUSSA JUMA
ANDREA NGOBOLE, PMT
Kampuni
ya Tanzanite One, imetoa msaada wa Sh 20 milioni kwa chama cha Madalali
wanawake,wanaouza madini ya Tanzanite mkoani Arusha .
Wakurugenzi wa kampuni hiyo, inayomilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO), Faisal Shabhai na Hussein Gonga walitangaza uamuzi huo wakati wakizungumza na madalali , katika ukumbi wa polisi jijini hapa.
Faisal
alisema kampuni yao ambayo inachimba Tanzanite, imetoa msaada wa sh 20
milioni,ili kuendelea kutekeleza mahusiano mema na wadau wa Tanzanite na
jamii ya wanawake ambao wanajihusisha na biashara ya kuuza madini hayo.
Alisema
msaada huo, umetokana na maombi ya wanawake hao, kusaidiwa waliyotoa
katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na viongozi wa
Tanzanite One.
Katika hatua nyingine kampuni hiyo imetenga kiasi cha sh 200 milioni kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali ya
kisasa Mererani.
kisasa Mererani.
Gonga
alisema kwa sasa tayari wametoa matofali 65,000 ambayo yapo eneo ambalo
itajengwa hospitali hiyo ili kuondoa matatizo ya ukosefu huduma za afya
katika mji wa Mererani.
Awali
Mwenyekiti wa chama hicho, Eugen Augustine alisema madalali wa madini
wanawake mkoani Arusha, wanakabiliwa na tatizo la mtaji mdogo na hivyo
kushindwa kunufaika na biashara yao.
Alisema kutokana na tatizo hilo, ndio sababu waliomba msaada kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha na Tanzanite One ili wasaidiwe.
Katika
hatua nyingine, Kampuni hiyo, imetoa msaada wa mahindi magunia 250 kwa
wananchi wakazi wa kata ya Naisinyai ikiwa ni sehemu ya mchango wa
kampuni hiyo kwa jamii inayozunguka migodi yake.
Faisal alisema msaada huo, utasaidia makundi maalum katika jamii na ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kushauri kampuni hiyo, iongeze misaada kwa jamii inayowazunguka.
kushauri kampuni hiyo, iongeze misaada kwa jamii inayowazunguka.
Kampuni ya Tanzanite One inamilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Sky Associate Ltd na shirika la madini la taifa(STAMICO).
Chanzo:Fullshangwe Blog





No comments
Post a Comment