Monday, March 27, 2017

TIMU YA TAIFA YA BURUNDI YATUA DAR ES SALAAM,MAVUGO NDANI


mavugo na burundi 3

Na.Alex Mathias,Dar es salaam

Msafara wa wachezaji pamoja na benchi la ufundi la timu ya Burundi umekwisha wasili Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupambana na Timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) katika mchezo wao wa kirafiki unaotarajiwa kupigwa kesho uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Timu hiyo iliwasili uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) mida ya saa nne asubuhi na kuelekea katika hoteli ya Southen Sun iloyopo jijini Dar es Salaam ambako watakuweka kambi yao hapo kwa ajili ya kusubiri siku ya mchezo ifike.
Ofisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF), Alfred Lucas alisema tayari wamekwisha wapatia ratiba ya mambo yote viongozi wa timu ya Burundi ambako kwa kuanza watapaswa kujitokeza na kuzungumza na waandishi wa habari saa tano asubuhi ya leo kabla ya kwenda kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa.
Alisema timu hiyo imepewa nafasi ya kufanya mazoezi katika uwanja wa taifa kabla ya kuanza kwa pambano lao la kirafiki kutokana na kanuni za mpira wa miguu kutaka timu mwenyeji kuiachia timu mgeni kutumia uwanja utakaotumiwa kwenye mchezo husika siku moja au mbili kabla ya kufanyika kwa mchezo.
“Wachezaji wetu wanaendelea na mazoezi kama kawaida na wamekwisha andaliwa kiakili na kimwili kupambana na  timu zote tutakazo cheza nazo michezo ya kirafiki na kwa siku tofauti tofauti,” alisema Lucas.
Pia Lucas aliwaeleza watanzania kutotazama rekodi ya timu wanayocheza nayo bali wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu hiyo ya taifa kwani kama itafanikiwa kushinda kwenye mchezo huo kutawapandisha mara kadhaa kwenye viwango vya Mpira wa miguu vinavyotolewa na Shikirikisho la Soka Duniani(FIFA).
Kwa Upande wake Nahodha wa Timu hiyo, Mbwana Samatta alisema wanakila sababu za kuibuka na ushindi katika mchezo wao huo kwani maandalizi yaliyofanyika yanaonesha hari na utayari mkubwa walionao wachezaji wa timu hiyo na pia watajitahidi ili washinde kama walivyo fanya kwa Botswana .
Alisema hawawezi kufanya masihara yoyote katika mchezo huo, kwani wanahitaji kupata ushindi wa aina yoyote ile katika mchezo wao huo na kutoka katika nafasi mbaya za msimamo wa soka zilizotolewa siku chache na FIFA.
Alidai sapoti ya watanzania ndio kitu pekee kitakachowapa nguvu ya kuibuka na ushindi na kuongeza kuwa hakuna haja ya kuweka ushabiki wala tofauti za aina yoyote katika mchezo huo wenye umuhimu mkubwa kwenye mustakabali wa soka la Tanzania.
“Niwaombe watanzania mjitokeze kwa wingi kwenye mchezo wetu wa kesho  na pia ningewaomba waweke tofauti zao pembeni na kuja kutushangilia vijana wao kwa kazi tutakayokwenda kuifanya kwani wao ndio kila kitu kwetu na tunawategemea sana kwenye kutupa sapoti,” alisema Samatta .
Chanzo:Fullshangwe Blog
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment