Writen by
sadataley
8:52 AM
-
0
Comments
Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi (katikati) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius Bw. Kevin Ramkaloan (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano katika utangazaji wa utalii wakati wa maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin Ujerumani. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo.
Mkurugenzi mwendeshaji wa Bodi ya Utalii Tanzania Bibi Devota Mdachi (katikati) na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius Bw. Kevin Ramkaloan (kushoto) wakisaini mkataba wa ushirikiano katika utangazaji wa utalii wakati wa maonesho ya Kimataifa ya utalii ya ITB Berlin Ujerumani. Anayeshuhudia kulia ni Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo.
Mwenyekiti wa TTB Jaji mstaafu Thomas Mihayo akibadilishana mawazo na Mkuu wa Idara ya mauzo ya shirika la ndege la Condor Bw. Andre Horn muda mfupi baada ya TTB na Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius kusaini makubaliano ya ushirikiano.
Na: Geofrey Tengeneza -Berlin
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Mamlaka
ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius zimetiliana saini mkataba wa ushirikiano
baina yao katika kutangaza wa nchi hizo mbili kwa pamoja katika baadhi
ya masoko ya masoko ya Marekani, China, Australia, India na masoko
mengine barani la Ulaya.
Mkataba huo uliosainiwa leo katika
maonesho ya Utalii ya ITB na wakurugenzi wakuu wa taasisi hizo ambao ni
Bi Devota Mdachi kwa upande wa Bodi ya Utalii Tanzania na Bw. Kelvin
Ramkaloan kwa upande wa Mamlaka ya Ukuzaji Utalii ya Mauritius una lengo
kuvutia watalii zaidi kutoka barani Ulaya, Amerika na Asia.
Akizungumzia mkataba huo Mkurugenzi
Mwendeshaji wa TTB Bi Devota Mdachi amesema kuwa katika mkataba huo
wamekubaliana kushirikiana katika kutangaza vivutio vya utalii vya nchi
hizo mbili sambasamba na kuhakikisha kuwa watalii wanaotembelea
Mauritius ambayo ni maarufu kwa utalii wa fukwe wanatembela pia Tanzania
kwa ajili ya utalii wa kutazama wa wanyama katika hifadhi zetu
mbalimbail za Taifa , kupanda mlima Kilimanjaro na kutembelea maeneo
mengine ya vivutio vya utalii.
“Tutazitangaza nchi zetu kama maeneo
pacha ya utalii lengo likiwa ni kutumia fursa ya watalii wanaotembelea
Mauritus kwa ajili utalii wa fukwe kuunganisha safari zao na
kujakutembela pia Tanzania kupitia shiika la ndege la Mauritus kwa ajili
ya kujionea vivtio vyetu kama vile wanyama , mlima Kilimanjaro, Bonde
la Ngorongoro, na vingine vingi ambavyo Mauritus hawana.” alisema Bi
Devota Mdachi.
Chanzo:Mjengwa Blog
No comments
Post a Comment