Writen by
sadataley
11:44 AM
-
0
Comments
VIONGOZI na wanasiasa katika kata ya Mdabulo wilaya ya Mufindi mkoani
Iringa wameonywa kuingiza siasa katika mradi wa maji uliofadhiliwa kwa
zaidi ya Tsh milioni 200 na shiriki lisilo la Kiserikali la Rural
Development Organization (RDO)
Onyo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza wakati akifungua mradi huo kwenye kijiji cha Ikanga juzi.
Alisema kuwa lengo la wafadhili wa RDO kusaidia mradi huo ni kutaka
kunusuru wananchi ambao walikuwa wakitabika na ukosefu wa huduma ya maji
safi na salama kwa muda mrefu hivyo hatapenda kusikia ama kuona
wanasiasa wanavuruga mradi huo kama walivyoanza kufanya hivyo awali .
Kuwa ofisi yake itawachukulia hatua kali wote ambao watabainika kuugeuza
mradi huo kuwa ni mradi wa kisiasa ama kuhujumu miundo mbinu ya mradi
huo .
" Nawapongeza sana wadau wetu wa maendeleo wilaya ya Mufindi RDO kwa
kusaidia mradi huu wa maji ni mradi mzuri uliotumia fedha nyingi hivyo
sipendi kuona siasa inaingizwa katika mradi huu naomba nipeni taarifa
kwa yeyote atakayeingiza siasa ili nimshughulikie .......na naagiza
utaratibu wa uendeshaji wa mardi ufuatwe ikiwa ni pamoja na wananchi
kuchangia mradi huo"
Hata hivyo alisema jitihada zinazofanywa na RDO katika wilaya ya Mufindi
na Kilolo ni kubwa na serikali inatambua mchango huo mkubwa wa kusaidia
huduma ya maji pia kusaidia kutoa elimu kwa watoto yatima.
Mratibu wa RDO Fidelis Filipatali alisema kuwa mradi huo umekabidhiwa
kwa jumuiya ya watumia maji inayojumuisha vijiji vilivyopo katika kata
yamdabulo (Kidete, Ludilo na Ikanga) yenye usajili namba 007 na kuwa
shirika la RDO tayari linausajili namba 00NGO/00007700 na ndio walezi
wakuu wa miradi hiyo ya maji.
Kuwa RDOMdabulo ikisaidiana na nguvu ya wananchi tangu mwaka 2013 kwa
lengo la kutatua changamoto za maji katika kata ya Mdabulo, Ihanu,Ifwagi
na Luhunga ikiwalenga hasawatoto yatima, akina mama na jamii nzima
inayowazunguka ilianza kazi hiyo ya kutafuta ufumbuzi.
Alisema wanafuaika na mradi huo ni taasisi zaidi ya 7 zikiwemo shule
pamoja na watu zaidi ya 1500 na kuwa wamefanikiwa kujenga tank kuu
Ludilo ambalo linapelekamaji ikanga na Kidete , kusafirisha maji
kutokakidete mpaka mtaa wa Redi, kutemelea vituo mbalimbalikwa kila
kijiji , ili kuweza kujilidhisha maendeleo ya mradi, maabara
inayotumikakupimia maji , kila baada ya miezi mitatu, kujisajili katika
bonde lamto RUFIJI (Rufiji basin) Wakati changamoto kubwa ni baadhi ya
watumiaji maji kutochangia michango,hivyo kumepelekea ugumu wa
uendeshaji wa mradi na kubaki kutegemea mlezi wetuambae ni RDO kwa kiasi
kikubwa,Siasa kutumika katika mradi, hivyo kumepelekeakuwepo na
uchagiaji mgumu wa michango ,viongozi kutowajibika ipasavyo katika
kuusimamia mradi wa maji,jamii kupuuzia Elimu wanayopta toka kwa
wataalamu hivyo kupelekea mradi kuwa tegemezi.
Mkurugenzi wa RDO Fidelis Filipatali akizungumza baada ya kuzindua Mradi wa maji
Mkurugenzi wa mradi wa maji wa RDO Fidelis Filipatali akisaidia kumtwisha ndoo ya maji mwanamke wakati wa uzinduzi wa mradi huo
Wananchi wakishiriki kusogeza bomba za maji
Mjumbe wa NEC wilaya ya Mufindi Marcelina Mkini ambae ni mwenyekiti wa
UWT Wilaya ya Mufindi akisaidiana na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina
Masenza kumtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Ikanga mara baada ya
uzinduzi wa mradi wa maji





No comments
Post a Comment