Writen by
sadataley
1:07 PM
-
0
Comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia
Mhe. Hailemariam Dessalegn ikulu jana Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Ethiopia Dkt. Workneh Gabeyehu wakisaini mkataba unaolenga ushirikiano
katika kupambana na uhamiaji haramu, masuala ya biashara na mapambano na
ugonjwa wa malaria Ikulu Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.
Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut
Teketel wakisaini mkataba wa makubaliano yanayotoa fursa za uwekezaji
pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof.
Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut
Teketel wakibadilishana mikataba wa makubaliano yanayotoa fursa za
uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini
Dar es salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari na kuwaeleza
masuala ambayo wamekubaliana kushirikiana na Serikali ya Ethiopia
Ikiwemo sekta ya Nishati, Usafiri wa Anga, Sekta ya Utalii, Sekta ya
Elimu pamoja na Sekta ya Maji kulia ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.
Hailemariam Dessalegn ikulu jana Jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam
Dessalegn akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya utiliaji
saini mikataba ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia ambao
amemuahidi kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali za maendejana,
Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli ikulu jana Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.
Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa
habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.
Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa
habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.
PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO
No comments
Post a Comment