Writen by
sadataley
9:23 AM
-
0
Comments
Donald Trump ziarani Bethlehem
Rais Trump wa Marekani anaendelea na ziara yake Mashariki ya kati. Amekutana na kiongozi wa utawala wa ndani wa Palestina Mahmoud Abbas na ataweka shada la mauwa katika kumbusho la Yad Vashem kabla ya kuelekea Vatikan.
Rais huyo wa Marekani amekaribishwa na Mahamoud Abbas katika kasri la rais mjini Bethlehem , baada ya mlolongo wa magari yaliyofuatana nae kupita katika njia unakokutikana ukuta uliojengwa na Israel pamoja pia na kivukio mashuhuhuri, kinachoamuru kufunguliwa njia ya kuingia Bethlehem. Kwa namna hiyo rais Trump amejionea mwenyewe ukweli wa hali ya mambo namna ulivyo katika mzozo mmojawapo mkongwe kabisa wa dunia.
Katika mazungumzo pamoja na waandishi habari mwishoni mwa mazungumzo yake pamoja na kiongozi wa utawala wa ndani wa Palestina mjini Bethlehem, rais Trump ameahidi "kufanya kila liwezekanalo" kuwasaidia waisrael na wapalastina kufikia makubaliano ya amani.
Wapalastina na Waisrael wako tayari kushirikiana na Trump kusaka amani
"Amani ndio chaguo tunalobidi kuwa nalo kila siku na Marekani tuko tayari kusaidia kuifikia ndoto hiyo" amesema rais Trump mbele ya kiongozi wa utawala wa ndani wa Palestina, Mahmoud Abbas, aliyekutana nae ana kwa ana hapo awali. Ameongeza kusema, Mahmoud Abbas amemhakikishia utayarifu wake wa kushirikiana kwa dhati ili kulifikia lengo hilo na kwamba waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pia amemhakikishia hayo hayo alipokutana nae jana.
Rais Trump amesema "makubaliano ya amani pamoja na Israel yatafungua njia ya kupatikana amani katika eneo lote la mashariki ya kati."Rais wa Marekani ametilia mkazo umuhimu wa kuufufua uchumi wa wapalestina anaosema uko katika hali mbaya kupita kiasi.
DW SWAHILI
No comments
Post a Comment