Writen by
sadataley
12:44 PM
-
0
Comments
Umoja wa Ulaya umeyaweka majina tisa ya viongozi wa ngazi za juu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa tuhuma za kuhusika na ukiukaji wa haki za binaadamu nchini humo.
Baraza la Umoja wa Ulaya EU limetoa taarifa na kusema kuwa limeweka majina matatu ya mawaziri wa serikali ya sasa na wengine wa zamani katika orodha ya vikwazo vyake. Kalev Mutondo, mkuu wa idara ya intelejensia ya kitaifa nchini humo (ANR) na pia Lambert Mende,
Msemaji wa Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao kwa sasa wako nchini Uchina, nao wamewekwa kwenye orodha hiyo ya vikwazo. Kwa ajili hiyo kuzuiwa mali za shakhsia hao na pia kupigwa marufuku kuingia nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya ni miongoni mwa vipengee vilivyotajwa katika vikwazo hivyo vipya. Afisa mmoja wa serikali ya Kinshasa ambaye hakutaka kutaja jina lake ametoa radiamali kuhusiana na hatua hiyo ya EU na kusema kuwa, lengo la vikwazo hivyo ni kuvuruga usalama na uthabiti wa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Mataifa, tangu mwaka jana hadi sasa zaidi ya watu 400 wameuawa katika eneo la Kasaï kutokana na mapigano baina ya jeshi la serikali na waasi huku watu wengine milioni moja na laki mbili na 70 elfu wakiwa wakimbizi. Mapigano mapya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yaliibuka baada ya Kamwina Nsapu, mmoja wa viongozi wa kikabila wa eneo hilo la Kasaï kuanzisha uasi dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
Parstoday
No comments
Post a Comment