Writen by
sadataley
9:48 AM
-
0
Comments
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusiana na tishio la mabadiliko ya tabianchi na kutoa wito wa nchi zote kuungana katika hilo.
Antonio Guterres amesema kuwa, kuna haja kwa nchi zote duniani kusimama kidete kuhusiana na suala zima la utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na tishio la mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, kinyume na serikali ya Marekani, nchi nyingine zinapaswa kusimama kidete kukabiliana na ukiukwaji wa makubaliano ya Paris Ufaransa kuhusiana na mabadiliko ya tabianchi.
Akizungumzia tishio la Rais Donald Trump wa Marekani la kujitoa nchi yake katika mkataba wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris Ufaransa, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, kama nchi fulani ina shaka na umuhimu wa makubaliano haya, basi ni jukumu la nchi nyingine kuungana katika hili.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, dunia ipo katika hatari na kama nchi hazitafanyia kazi makubaliano ya mkutano wa Paris juu ya mabadiliko ya tabianchi, basi hali itakuwa mbaya zaidi.
Makubaliano ya kwanza ya kimataifa ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi yalitiwa saini mwaka 2015 katika mkutano wa Paris, mji mkuu wa Ufaransa kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa karibu nchi 200 duniani. Rais wa sasa wa Marekanio Donald Trump amekuwa akiyakosoa makubaliano hayo na kuyataja kuwa ni kikwazo kwa mipango yake ya kiviwanda.
Parstoday
No comments
Post a Comment