Monday, May 22, 2017

Lindi: Kiongozi wa mbio za mwenge agoma kuzindua mradi

Lindi. Kiongozi  wa  mbio za  mwenge, Amour Amour ametakaa  kukagua mradi  wa  kikundi  cha vijana  changamkia  fursa cha ufugaji  wa  nyuki jimbo  la  Mtama  (VICHASCO)baada  ya  viongozi wa kikundi hicho  kutoa  taarifa  za  uongo  ikiwemo  umri wao.

Mradi  huo  unaojumuhisha  vijana  zaidi  ya  15  wanaofanya  shughuli  za  kufuga  nyuki , utengenezaji  wa thamani na ufyatuaji  wa  tofali  umeshindwa  kukaguliwa  baada  ya   watendaji kutoa  taarifa  zisizo  sahihi.

Awali  kabla  ya  kukaguliwa  mradi  huyo wanakikundi  wajilitambulisha  kwa   kiongozi  wa  mbio  za  mwenge ndipo  alipoanza kubaini  kuwa anadanganywa  baada  ya  mwenyekiti  wa  kikundi  hicho Mohamedi  Magongo (38) na Mnole Hasani (37) kudanganya   umri  wao kuwa  wao  ni  vijana  wakati umri wao umepita ujana.

Amour  amesema utambulisho  wa kikundi unaonyesha kuwa  ni  kikundi  cha  vijana lakini baadhi ya wanachama  na  viongozi  wa kikundi wana umri  mkubwa uliopita wa ujana.

Amesema ameshindwa  kukagua  mradi  huyo kutokana  na kutoridhishwa  na  taarifa  za  awali  zilizotolewa  na   viongozi wa kikundi  ambazo  tayari zimempa  wasiwasi kuwa  hata  taarifa  zingine  zitakuwa  za kupikwa.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment