Monday, May 22, 2017

Marekani: Operesheni zetu za kijasusi zimefeli nchini China

Gazeti moja la nchini Marekani limetangaza kuwa, serikali ya China imefanikiwa kuzima operesheni zote za Shirika la Kijasusi la Marekani CIA.
Gazeti la Washington Post la nchini Marekani limeandika: Mwaka 2010, China iliwaua au kuwafunga majasusi wa CIA nchini humo na kusambaratisha mtandao wa kijasusi wa Marekani, hivyo imezima muundo wote wa kukusanya taarifa za kijasusi uliokuwa unafanywa na majasusi wa Marekani nchini China.
Kwa mujibu wa gazeti hilo, viongozi wa hivi sasa na wa huko nyuma wa Marekani wanasema kuwa, kushindwa operesheni za kijasusi za Marekani nchini China katika miongo ya hivi karibuni ni moja ya kufeli kubaya kabisa nchi hiyo na baadhi ya viongozi hao wa Marekani wanaamini kuwa CIA inafanya usaliti.
Ujasusi

Baadhi ya maafisa wa masuala ya usalama wa Marekani wanasema, China imefanikiwa kudukua na kupenya kwenye mfumo wa mawasiliano ya siri wa Shirika la Kijasusi la Marekani CIA na kujua siri na mipango ya shirika hilo. 
Gazeti la Washington Post aidha limewanukuu viongozi wa zamani wa Marekani wakisema kuwa, katika wiki za mwishoni mwa mwaka 2010 hadi mwishoni mwa mwaka 2012, serikali ya China iliua majasusi wasiopungua 12 Marekani na kuwatia mbaroni majasusi takriban 8 hadi 10 wa CIA.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment