Writen by
sadataley
2:43 PM
-
0
Comments
Ndugu zangu,
Itakumbukwa, kwenye kampeni zilizopita za Uchaguzi Mkuu wa Marekani kuna kubwa lilitokea. Ni kwenye kusanyiko la chama cha Republican.
Itakumbukwa, kwenye kampeni zilizopita za Uchaguzi Mkuu wa Marekani kuna kubwa lilitokea. Ni kwenye kusanyiko la chama cha Republican.
Ted Cruz, aliyepata kuwania tiketi ya kugombea Urais aliwashangaza wafuasi wa Republican, tena hadharani, na bila kupepesa macho au kumung'unya maneno, alipotamka kwa ujasiri mkubwa kuwa hawezi kumthibitisha Donald Trump kama mgombea urais kwa tiketi ya chama chake.
Sababu yake ilikuwa ni moja na kwa kwake Ted Cruz ni ya msingi; kuwa hawezi kumthibitisha mtu aliyemtukania mkewe na baba yake mzazi.
Donald Trump aliwahi kuzungumzia hadharani mwonekano wa mke wa Ted Cruz na akaenda mbali hadi kumtuhumu baba mzazi wa Ted Cruz kuwa alihusika kwenye njama za kumwua JF Kennedy.
Na hakika, hilo la mwisho limenifanya niwarudishe tena kwenye simulizi ya kusisimua ya JF Kennedy ambaye, mzimu wake unaonekana kuendelea kuitafuna Marekani hadi hii leo.
JF Kennedy ni nani?
Duniani kuna wanasiasa walioamsha hamasa za wengi kupenda siasa. Kwangu mimi binafsi, JK Nyerere na JF Kennedy ni miongoni mwa wanasiasa hao.
Miaka 54 imepita tangu JF Kennedy auawe. Novemba 2 , 1960 ndio siku ambayo John F Kennedy alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani.
Alikuwa Rais wa 35 akiwa na miaka 43 tu, hivyo, Rais wa pili kijana kuliko wote katika Marekani.
Ni rais wa kwanza wa Marekani kuzaliwa katika miaka ya 1900. Na Rais wa kwanza Mkatoliki kuliongoza taifa la Marekani. Ni baada ya siku elfu moja na thelathini na sita Ikulu ndipo alipouawa, Novemba 22, 1963. Na miaka mitano baadae, nduguye, Bobby Kennedy, naye aliuawa.
JF Kennedy na JK Nyerere walikuwa marafiki.
Maggid,
Iringa.
Chanzo:Mjengwa Blog

No comments
Post a Comment