MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MNEC) Mwanasheria Ridhiwani Kikwete juzi amewaaga wanachama wa chama hicho kwa kuwamwagia kitita cha sh. Mil. 20 zitazotumika kwa ajili ya chaguzi zinazotaraji kuanza wiki hii.
Ridhiwani ametoa kauli hiyo kwenye Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani kilichofanyika kwa siku mbili katika shule ya Sekondari ya Lugoba ambapo alisema hatua hiyo ni shukrani yake kwa wana-CCM hao walioonesha imani kwake katika kipindi cha miaka mitano.
Chini ya Mwenyekiti wa chama hicho wilaya Almass Masukuzi, Katibu Kamote Kombo, Mbunge jimbo la Bagamoyo Dkt. Shukuru Kawambwa na viongozi mbalimbali, Ridhiwani alisema kuwa amefurahishwa kwa ushirikiano uliokuwepo katika kipindi hicho, hivyo ameamua kwa mapenzi yake mwenyewe kukitunuku hicho kiasi hicho.
"Nina faraja kubwa kukutana na wanachama wenzangu ambao pamoja tumetekeleza kwa vitendo majukumu ya kukiimarisha chama chetu, natumia mkutano huu kuwaaga rasmi kutokana na mabadiliko ya uendeshaji mpya kichama, naahidi kuchangia sh. Mil. 20 zitakazotumika katika kufanikisha chaguzi zinazotaraji kuanza wiki hii," alisema Ridhiwani.
Alieleza kwamba fedha hizo zitakwenda katika Kata zote 26 ambapo kila moja itapata sh. Laki 2, pia katika matawi 295 kila moja litapokea sh. 50,000 zitazosaidia zoezi la chaguzi kuanzia ngazi husika na hatimae ngazi zinazofuata za juu yake.
"Imani yangu ni kwamba kiasi hicho japo ni kidogo lakini kitasaidia kupunguza changamoto za kiuchaguzi, hivyo imani yangu ni kwamba zitafika maeneo lengwa na hatimae malengo yetu ya kufanikisha chaguzi hizo zitafanikiwa," alisema Mwanasheria huyo huku akishangilia na wanachama hao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Masukuzi aliwataka wanachama hao kujipanga katika kufanikisha mchakato huo na hatimae kupatikana kwa viongozi wataokivusha kwenye chaguzi zinazofuata hapo baadae.
"Niwaombe wanachama we zangu tuwe makini katika kipindi hiki cha kuwlekea kwenye chaguzi zilizo mbele yetu, imani yangu wote tupo tayari katika lufanikisha chaguzi hizo hivyo kila mmoja ahakikishe anatumia vema haki yake ya kuchagua na kuchaguliwa kwenye nafasi mbalimbali za uongozi," alisema Masukuzi.
No comments
Post a Comment