Saturday, May 6, 2017

Serikali kuagiza sukari nje ya nchi

Serikali ya Tanzania imeiagiza Bodi ya Sukari nchini(SBT) kuagiza Sukari nje ya nchi kutokana na upungufu uliosababishwa na kufungwa kwa viwanda.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya utafiti uliofanywa kuonyesha kuwa bei ya sukari nchini imepanda katika maeneo mbali mbali, huku bei ikiwa kati ya shilingi 2600/- mpaka kiasi cha shilingi 3000/-.

Mnamo mwaka jana SBT ilipanga bei elekezi ya sukari kuuzwa kwa kiasi cha shilingi 1.800/- kwa kilo, lakini inaonyesha agizo hilo halikufuatwa na wauzaji pamoja na wasambazaji wa bidhaa hiyo.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment