Writen by
sadataley
12:24 PM
-
0
Comments
Mtandao wa Global Research umeandika kuwa, serikali ya Marekani daima imekuwa muungaji mkono mkuu wa makundi ya kigaidi.
Ripoti ya Global Research imesema: Wakati Iran daima imekuwa ikikabiliana na kupambana na makundi ya kigaidi, wanasiasa wa Marekani wamekwenda kinyume na kuyaunga mkono makundi hayo na kufanya jitihada za kuzusha ghasia na machafuko nchini Iran.
Rupoti hiyo imesisitiza kuwa, sera za Marekani huko Iraq na Syria pia ni kuyaunga mkono na kuyasaidia kwa pande zote makundi ya kigaidi.
Ripoti hiyo ya Global Research imetolewa kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa na kundi la kiwahabi la Daesh Jumatano iliyopita mjini Tehran na kuua watu 17. Watu wengine 52 walijeruhiwa.
Kundi hilo la kigaidi la Daesh (ISIL) lilianzishwa kwa msaada wa Marekani, Saudi Arabia, Uturuki, Israel na washirika wao na linatumiwa kwa shabaha ya kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar Assad wa Syia na kuvuruga hali ya mambo nchini Iraq.
Parstoday
No comments
Post a Comment