Monday, June 12, 2017

Kikwete kuchekelea na mradi wa Dola milioni 15

MRADI mkubwa wa maji kutoka chanzo cha Mto Wami Halmashauri ya Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani nchini Tanzania unaotaraji kugharimu Dola za Kimarekani Mil. 15, una malengo ya kuwawezesha wanakikundi cha KIPA kuweza kulima zao hilo kwa msimu mzima wa mwaka.

Umoja huo unaoundwa na Wakulima wa zao la Mananasi Kiwangwa (Kiwangwa Pinaple Association) unatafuta fedha hizo kwa lengo la kuweza kuvuta maji kutoka chanzo cha Mto wa Wami wilayani humo utaowawezesha wana kikundi hao kuwa na uhakika wa kulima zao hilo katika kipindi chote cha mwaka ulikinganishana hivi sasa ambapo wanasubiri msimu wa mvua pekee.

Rais Mstaafu wa Serikali ya awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete aliyasema hayo juzi wakati mwandishi wa habari alipofika kijijini kwake Kiwangwa anakomiliki eka 200 za mazao mbalimbali, kati ya hizo zilizokuwa zimeshapandwa zikiwa 64 ambazo kwa sasa zipo katika hatua za kuzipalilia.

Dkt. Kikwete alisema kuwa umoja wao tayari umeanza mikutano ya kuhusu gharama za mradi huo kutoa chanzo cha Maji cha Mto Wami na kuufikisha eneo la hilo unaotaraji kutumia Dola Mil. 15 na kwamba ndio wameanza mchakato wa kutafuta fedha hizo zitazofanikisha zoezi hilo litalosaidia wanachama kulima zao hilo kwa msimu wa mwaka mzima.

"Tayari vikao vimeshaanza vya kupanga namna kupata fedha hizo, lengo kuu ni kuhakisha tunakuwa na mradi mkubwa wa umwagiliaji utaosaidia sisi wanachama kuweza kulima zao hili wakati wote badala ya kusubiri kipindi cha mvua tu, kwa hatua hiyo utatusaidia sana wanachama kuwa na uhakika mkubwa wa kujiongezea kipato kupitia kilimo hicho," alisema Dkt. Kikwete.

Akizungumzia uboreshaji wa zao hilo kisasa zaidi, Dkt. Kikwete alisema wapo kwenye matayarisho ya kuleta miche mipya ya kisasa ya zao hilo na kwamba  iliyopo hivi sasa inaitwa Smoth Kayan mbegu ambazo mananasi yake huwezi kuuza nje na kuwa yanayotakiwa nje ni MD 2 ambayo ndio wanaangaika nayo na kuwa mradi wao unakwenda vizuri.

"Tutawatumia watalamu wetu wa kilimo walioko Arusha na Morogoro kuwapatia elimu wakulima wetu namna ya kuzalisha zao hilo kwa wingi, lakini si hivyo tu pia tukiweza kumwagilia kitachotokea ni kwamba tutakuwa na uwezo wa kulima kipindi chote cha mwaka mzima hivyo kuboresha zaidi ki, omo na nsoko kwa ujumla," aliswma Mstaafu huyo.

Akizungumzia hali ya kilimo ukanda wa mikoa ya Pwani, Dkt. Kikwete alieleza kuwa palizi ndio tatizo kubwa ukilinganisha na kilimo chenyewe huku akifafanua kwamba hali hiyo inatokana na eneo husika kuwa na joto kali hali inayozalisha unyevunyevu hivyo majani kukua kwa kasi kubwa.

"Kutokana na hali hiyo utakuta mkulima anaacha shamba lake kwa muda ili akianza palizi aweze kufanya kwa wakati mmoja, utakuta mkulima anapalilia, akiwa katikati ya shamba huku nyuma majani yamejaa utadhani hajapalilia, kama mtu unapita kipindi hicho anaweza kusema mkulima mvivu kumbe si hivyo hali ya hewa inasababisha majani kujaa mashambani," alimalizia Mstaafu huyo.

Aidha alisema eneo la Msoga ana shamba kubwa la Mahindi kwa ajili ya mifugo yake tu ambapo ametumia mbegu ya mahindi ya njano ambayo kwa ng'ombe wa maziwa yanamwezesha kuwa na nguvu hivyo kutoa maziwa ya kutosha.

"Watu wanapopita wanasema Mzee tunasubiri kuja kubuna lini tuje, nawaambia hapana haya mahindi ni kwa ajili ya ng'ombe wangu tu, basi hawanielewi kabisa yaani nalima ajamba kubwa napanda mahinsi kwa ajili ya mifugo! unapomlisha ng'ombe mahindi ya njano yanmwezesha kiwa na nguvu hivyo kutoa maziwa menhi zaidi
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment