Tuesday, June 13, 2017

MTAJI ALIOTOA WAZIRI NCHEMBA WABADILISHA MAISHA YA VIJANA WA IRAMBA MAGHARIBI

Kikundi cha wajasilimia vijana 21 kutoka kata ya Ndulungu ambao walipewa pikipiki mbili na mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba  mwaka 2014 maisha yao yamebadilika baaada ya kutumia mtaji huo vizuri.
Vijana hao ambao walijiwekea malengo ya kuhakikisha kila mwezi wanakusanya kiasi cha fedha kisichopungua laki tatu kwa pikipiki mbili, mpango ambao uliwawezesha kupata fedha na kukunua pikipiki ya tatu.
Akizungumzia mafanikio yao, katibu wa kikundi hicho, Bakari Mohammed alisema baada ya muda vijana hao waliweza kutunza fedha na kupata fedha ambazo ziliwawezesha kununua gari aina ya Noah kwa milioni sita na laki tano.
Naye Mbunge wa Iramba Magharibi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema amefurahishwa na kitendo cha vijana hao kufikia mpaka kununua gari hiyo kwani kuna kikundi cha vijana aliwapa pikipiki lakini hawakufika mbali na mradi wao ukafa.
Waziri Mwigulu amewahidi kuwa endapo kikundi hicho cha vijana 21 watataka kununua gari aina ya Costa au Hiece wakiwa na fedha nusu ya kununua gari basi nusu nyingine atawapa kwasababu amewafurahisha sana kwa walilolifanya vijana hao.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment