Writen by
sadataley
12:28 PM
-
0
Comments
Kiongozi wa zamani wa waasi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Bosco Ntaganda hatimaye atapandishwa kizimbani Jumatano ijayo katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kujibu tuhuma za kutumia watoto kama wapiganaji vitani na kuwatumia mateka wa kike kama watumwa wa ngono.
Ntaganda ambaye ni mashuhuri kwa jina la "The Terminator" au Muangamizaji, atapandishwa kizimbani kujibu mashtaka kwamba wapiganaji wa kundi lake waliua na kunajisi raia wakati kundi hilo lilipovamia eneo lenye utajiri wa madini ya dhahabu la Ituri kuanzia mwaka 2002 hadi 2003.
Bosco Ntaganda mwenye umri wa miaka 43 amekanusha tuhuma 13 za kutenda jinai za kivita na jinai dhidi ya binadamu zilizofanywa na kundi lake la FPLC la wanamgambo wa kabila la Hema dhidi ya watu wa jamii ya Lendu na jamii nyingine.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, mapigano yanayoendelea katika mkoa wa Ituri huko kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamesababisha vifo na mauaji ya watu wasiopungua elfu 60 tangu mwaka 1999.
Parstoday
No comments
Post a Comment