Sunday, June 4, 2017

Real Madrid watwaa kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya

timu ya soka ya Real Madrid ya Uhispania imeicharaza Juventus ya Italia mabao 4-1 na kushinda kombe la Ligi ya Klabu Bingwa barani Ulaya. Mreno Cristiano Ronaldo alikuwa mwiba kwa kibibi kizee cha Turin baada ya kupachika mabao mawili katika mchezo huo wa fainali.
Juventus, waliokuwa wameanza vyema mechi hiyo walikomboa bao la kwanza la Ronaldo dakika ya 27 kupitia Mario Mandzukic na kufanya mambo kuwa sare wakati wa mapumziko lakini kipindi cha pili mawimbi yaliwageuka.
Mtanange huo wa fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya uliotazamwa pia na mabilioni ya watu kupitia runinga ulipigwa katika uwanja wa Cardiff mji mkuu wa Wales nyumbani kwa winga wa real Madrid Gareth Bale ulikuwa wa 19 kwa klabu hizo mbili kukutana.
Real Madrid wamefanikiwa kuwa klabu ya kwanza tangu AC Milan (1989, 1990) kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya/Kombe la Ulaya misimu miwili mfululizo, na ni mara yao ya 12 kushinda kombe hilo.

Mwaka huu ni mara ya tatu kwa Real Madrid kufika fainali katika misimu minne.
Juve ndiyo klabu pekee ambayo ilikuwa haijashindwa mechi yoyote msimu huu Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, klabu ya kwanza tangu Atletico Madrid mwaka 2013/14 kufika fainali bila kushindwa.
Real Madrid nao walikuwa wamefunga kila mechi kati ya mechi 12 walizocheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu huu.
Kushindwa kwa Juventus ni pigo kubwa kwa nahodha wao, mlinda lango Gianluigi Buffon, 39, ambaye hajawahi kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment