Monday, July 10, 2017

Baraza la Mawaziri la Uingereza lagawanyika kuhusu suala la kujiondoa EU

Baraza la Mawaziri la Uingereza limekumbwa na hitilafu kuhusu namna nchi hiyo itakavyojiondia katika umoja wa Ulaya na matukio yatakayojitokeza kufuatia hatua hiyo.
David Davis, Waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya Brexit
Gazeti la Independent linalochapishwa nchini Uingereza limeandika kuwa kila waziri katika serikali inayoongozwa na Bi Theresa May Waziri Mkuu wa nchi hiyo hadi sasa ameonekana kuwa na mitazamo tofautii kuhusu suala la kujiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya. Gazeti hilo limeashiria matamshi ya Philip Hamond Waziri wa Fedha wa Uingereza aliyesema kuwa, London inapasa kulinda siasa zake za kibiashara baada ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya. Hii ni katika hali ambayo David Davis Waziri wa Uingereza anayehusika na masuala ya Brexit amekuwa akisisitiza kuwa, nchi hiyo haitakuwa katika Soko la Pamoja au katika  Muungano wa Forodha wa Ulaya.
 Gazeti la Independent limeendelea kuandika kuwa, London bado haijadiriki uhakika wa mambo na inaendelea kuwa na wasiwasi na kutilia shaka kura ya maoni kuhusu kujiondoa Uingereza katika Umoja wa Ulaya licha ya kupita zaidi ya mwaka mmoja tangu kufanyika kura hiyo. 
Parstoday
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment