Thursday, July 6, 2017

Haya hapa Mashtaka aliyosomewa Yusuf Manji Kitandani Muhimbili alipolazwa


SERIKALI imemsomea Mashtaka saba Mwenyekiti wa Quality Group Yusuf Manji na wenzake watatu yakiwamo ya Uhujumu uchumi na usalama wa nchi

Kesi walisomewa Kwenye Hospitali ya Muhimbili Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete alipolazwa Mtuhumiwa namba moja Yusuph Manji Mbele ya Hakimu Mkazib wa mahakama ya Kisutu Huruma Shahidi Wakili wa Serikali Kishenyi Mitalemwa aliwaomea washtakiwa mashataka yao.

Watuhumiwa wengine ni Pamoja na Abdala Sangey,  Deogratias Kisimba, na Tobias Fwele

Shitaka la Kwanza Tarehe 30 Juni 2017 eneo la Chang'ombe  Temeke Jijini Dar es Salaam walikutwa na Askari Polisi  wakiwa na mabunda 35 ya vitambaa yanayotumika kutengenezea Sare  za Polisi zenye Thamani ya Milioni 192.5

Shitka la Pili watuhumiwa wote Tarehe 30 Juni walikutwa na Mabando Manane ya vitaambaa vinavyotumika kutengeneza sarea za JWTZ

Kosa la Tatu  washtakiwa wote  kwa pamoja tarehe 1 July  walikutwa na mihuri ya jeshi la Tanzania iliyoandikwa  "Mkuu wa Kikosi 121 Kikosi cha jeshi JWTZ "bila kuwa na uhalali kitendo kinachohatatisha usalama wa nchi

Kosa Nne watuhumiwa walikutwa na Mhuri  wa JWTZ  yenye maandishi  Kamanda kikosi 834 KJ makutupola Dodoma bila kuwa na uhalali kitendo


Shitaka la tano kukutwa na Mhuri wa Serikali wenye maneno "COMMANDING Oficcer 835 Kj Mgambo P.O.BOX..."

Shitaka la sita kukutwa na mali inayozaniwa kupatikana isivyo halali Tarehe 1 Julai Chang'ombe Plat namba SU 383 ambayo ilipatakana isivyo halali.

washtakiwa Hawakuruhusiwa kujibu mashtaka hayo kwa sababu wanastakiwa kwa sheria ya Uhujumu Uchumi na usalama wa taifa.

Hakimu Shahidi amesma  Kwamba masuala hayo yasikilizwe kwenye Mahakama yenye mamlaka.
kesi hiyo itatajwa tena Tarehe 19 mwezi Julai  upelelezi wa Kesi haujakamilika.  
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment