Tuesday, August 22, 2017

Marekani: Watu wanane wafariki katika mashambulizi Chicago

Watu wanane wafariki katika matukio tofauti mjini Chicago nchini Marekani

Watu wanane waripotiwa kufariki katika matukio tofauti  katika jiji Chicago ambalo limepewa jina la mji mkuu wa uhalifu nchini Marekani.

Watu wanane wamefariki na wengine 54 wamejeruhiwa  mwishoni mwa Juma katika matukio tofauti.

Polisi ya kulinda usalama mjini Chicago Ijumaa imetoa ripoti kuhusu mashambulizi tofauti yaliotokea katika mji huo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo watu  wanane waliuawa na wengine 54 kujeruhiwa Kusini mwa Chicago.

Ifahamike kuwa mjini Chicago watu wapatao 422 waliuawa na wengine 2013 walijeruhiwa tangu kuanza kwa mwaka 2017.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment