Writen by
sadataley
3:57 PM
-
0
Comments
- Uhuru Kenyatta wa Jubilee ana kura 7,915,044 (54.35%)
- Raila Odinga wa ODM ana kura 6,520,918 (44.78%)
Kura zilizoharibika kufikia sasa ni 387,959.
Tume ya uchaguzi yaweka wazi fomu za matokeo
Tume ya Taifa ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kutoa fomu za matokeo ya vituo vya kupigia kura maarufu kama Fomu 34A.
Muungano wa upinzani ulikuwa umelalamikia kukosekana kwa fomu hizo na kusema ilikuwa vigumu kukagua matokeo yaliyokuwa yakipeperushwa katika mtandao wa tume hiyo.
Mwenyekiti wa tume hiyo Bw Wafula Chebukati amewaambia wanahabari kwamba meza maalum itatengwa katika kituo kikuu cha kujumlishia matokeo ukumbi wa Bomas, Nairobi kwa ajili ya maajenti wa vyama ambao wangependa kukagua fomu hizo
Aidha, ameongeza kwamba fomu hizo zitapakiwa kwenye tovuti ya tume hiyo. Tayari baadhi zimeshapakiwa.
BBC
No comments
Post a Comment