Rais Yoweri Museveni wa Uganda aitamani kampuni ya ndenge Tanzania kwa jinsi ilivyofanikiwa kurudi kwakasi, na kusema naye yupo mbioni kufufua shirika lao.
Rais Museveni aliyasema hayo alipokuwa nchini Tanzania kwa ajili ya shughuli ya uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima nchini Uganda, mpaka Tanga Tanzania, na kusema anaipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada za kurudisha ATCL, hivyo na yeye yuko mbioni kufufua shirika la ndege la nchi yake Uganda.
"Tunataka kutoa hongera kwa Watanzania, tunasikia mmerudisha kampuni yenu ya ndege, na sisi hivi karibuni tutafufua kampuni yetu ya ndege, kwa hiyo hizi kampuni za ndege tutafaidika kwa kutumia mafuta ambayo hayapo kwenye gharama kali (yatakayosafirishwa kupitia bomba hilo)", alisema Museveni.
Shirika la ndege la Tanzania lilikufa kwa miaka mingi, lakini baada ya kuingia Rais Magufuli alilifufua, na mpaka sasa linafanya kazi likiwa na ndege tatu, huku shirika la ndege ATCL likitarajia kuleta ndege zingine kubwa aina ya Boeing 787 Dash 8 Dreamliner
No comments
Post a Comment