Sunday, September 10, 2017

Manara afungukia uwekezaji wa Azam FC

Klabu ya Azam imeendeleza ubabe wake kwenye uwekezaji nchini, baada ya kuanzisha sehemu maalum ambayo waandishi wa habari (Media Center) watakuwa wakifanya kazi zao kwa wepesi.

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amesema uwekezaji ambao unafanywa na Azam sio wa kuubeza kutokana na klabu hiyo kuwa ya kitofauti Afrika Mashariki.

“Klabu hii haina miaka mingi lakini uwekezaji ambao wanazidi kuufanya, ni mkubwa ambao wametushinda mpaka sisi ambao bado tupo na vichaka na mabwawa yetu,” Haji Manara.

Manara aliongeza uwekezaji ambao unafanywa, unabidi kumshawishi muwekezaji kwa kupata matokeo na sio vitu vingine.

“Uwekezaji wa namna hii unahitaji matokeo kwasababu tajiri anayewekeza anahitaji furaha ya matokeo na sio vinginevyo.”

Wakati huohuo CEO wa Azam, Abdul Mohammed alifunguka licha ya kukamilisha sehemu hiyo bado wanataka kutengeneza makumbusho ya timu yao.

“Baada ya kukamilisha suala hili tuna jambo jingine ambalo tunataka kulikamilisha, tunataka tuwe na makumbusho yetu ambayo itakuwa inaelezea kila kitu kuhusu klabu yetu, hadi magari na jezi ambazo zilitumika tangu kuanzishwa kwa klabu hii,” Abdul Mohammed.
« PREV
NEXT »

No comments

Post a Comment