Writen by
sadataley
4:06 PM
-
0
Comments
“Tumeokolewa kwa Neema ya Mungu” ni kauli mbiu iliyochaguliwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuongoza maadhimisho ya Miaka 500 ya Matengenezo ya Kanisa 2017. Ifuatayo ni KKKT ratiba ya Juma la Matengenezo kuanzia ngazi ya sharika hadi kitaifa:
NGAZI YA DAYOSISI
Kamati inaafiki Azimio la kuwa na bustani ya miti lenye ua kama ilivyo nembo ya Dkt. Martin Luher na baada ya majadiliano ilipatana mambo haya ya ziada:
- Pawepo bustani au shamba la miti kwa kumbukumbu hiyo Kidayosisi /au Sharikani
- Maadhimisho yafanywe na Dayosisi, Sharika na Vituo vyote vya Kanisa
- Kwaya zote zijiandae kwa wimbo wa halaiki
- Kwaya zote zijiandae kwa tamasha la uimbaji
- Juma la kumbukumbu ya miaka 500 ya matengenezo ni tangu 1 – 8 Octoba 2017
NGAZI YA SHARIKA NA VITUO
1 Oct Jumapili
1 Oct Jumapili
- Iwe ni Siku ya mwanzo ya juma la maadhimisho
- Ibada maalumu ifanyike
- Mtaalamu awepo kufundisha kusudi na historia ya Matengenezo ya Kanisa
- Tamasha la Uimbaji
2 Oct Jumatatu
- Iwe ni Siku ya Vijana
- Miti ipandwe
- Kujitolea damu inapowezekana
- Watembelee watu walio na uhitaji katika jamii
3 Oct Jumanne
- Iwe ni Siku ya Wanaume
- Wanaume na Huduma za Udiakonia
- Maombi kwa wagonjwa
- Usafi wa mazingira
- Kongamano la wanaume na wavulana
4 Oct Jumatano
- Iwe ni Siku ya Wanawake
- Wanawake na Huduma za Udiakonia
- Maombi kwa wagonjwa
- Usafi wa mazingira
- Kongamano la wanawake na wasichana
5 Oct Alhamisi
- Iwe ni Siku ya Vituo vya Kanisa ngazi zote
- Vipindi vya dini mkazo uwe kuhusu matengenezo
- Watoe huduma za kijamii
- Wapate maelezo ya kusudi na historia ya matengenezo
- Utoaji damu inapowezekana
6 Oct Ijumaa
- Iwe ni Siku ya Watoto
- Mchungaji aongoze Ibada ya Watoto
- Igizo
- Kwaya au nyimbo
7 Oct Jumamosi
- Iwe ni Siku ya Watu wote
- Usafi wa mazingira
- Tamasha la uimbaji
8 Oct Jumapili
- Iwe ni Siku ya Kilele
- Ibada iwe ni moja tu inapowezekana
- Kwaya ya halaiki iimbe siku hiyo
- Tamasha la Uimbaji
NGAZI YA KITAIFA
- Kanisa limeteua Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira (TUMA) kuwa eneo la kuadhimisha miaka 500 ya matengenezo kitaifa.
- Kongamano la kitaifa litafanyika 7/10/2016 ambapo mada mbalimbali zitatolewa na kujadiliwa na wajumbe toka dayosisi 25 za KKKT.
- Tarehe 8/10/2017 itafanyika ibada maalumu ya kilele cha miaka 500 ya matengenezo.
IMETOLEWA NA ELCT website
No comments
Post a Comment